Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kuelekea Mkutano wa M300: Tanzania Yaweka Historia Uunganishaji Umeme Vijijini
Frank A. Mugogo 172

Kuelekea Mkutano wa M300: Tanzania Yaweka Historia Uunganishaji Umeme Vijijini

Kuelekea mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika, Tanzania imeweka historia kwa kufikisha huduma ya umeme kwa asilimia 78.4 ambapo kwa vijijini uunganishaji umefikia asilimia 100 na kwenye vitongoji umefikia asilimia 52.3 huku ikitarajiwa kuwa Watanzania milioni 13.5 watasambaziwa umeme ifikapo 2030.

Mha. Olotu amesema kuwa  idadi ya watu nchini baada ya kufanyika Sensa  ya Watu na Makazi iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni 60 na kwa taarifa ya umeme asilimia 78.4 ya watanzania wameunganishwa na umeme. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mha. Jones Olotu jijini Dar es Salaam. 

Amesema kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesema kuwa vijiji vyote 12,318 ambayo ni sawa na asilimia 100 vimefikiwa na umeme.

Aidha, Tanzania Bara ina jumla ya vitongoji 64,359 ambapo tayari vitongoji 33,657 sawa na asilimia 52.3 vimefikiwa na umeme na vitongoji 30,702 vilivyobaki vipo kwenye mpango wa kupatiwa umeme. 

Ameongeza baadhi ya faida za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuongezeka idadi ya  Watanzania watakaounganishwa na umeme ifikapo mwaka 2030 hadi kufikia milioni 13.5 kutoka milioni 5.2 ya sasa.

Ameongeza kuwa, Wakuu wa Nchi 54 kutoka Bara la Afrika na viongozi wengine watashiriki mkutano huo wakiwemo Mawaziri wa Fedha na Nishati kutoka barani Afrika.

Ameongeza kuwa, mkutano huo unafanyika nchini kwa sababu Rais Samia ni kinara wa nishati safi ya kupikia duniani na katika sekta nzima ya nishati Rais Samia amefanya mengi kwa watanzania. 

Mkutano huo utaenda sambamba na Maonesho yatakayofanyika tarehe 27 na 28 Janauari, 2025 katila ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma
 

Share

Print
«April 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
311234
CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

The Rural Energy Agency issue the Second Call for applications from qualified suppliers to Supply and install Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions through on-call basis.

Read more
56
789
Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Please find the attached Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24:

Read more
10111213
14
Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amuopengeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi kubwa ya kufikisha umeme vijijini hali iliyobadili maisha ya wananchi vijijini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top