Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe
Frank A. Mugogo 857

REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na kampuni ya Oryx Gas Tanzania, tarehe 12 Februari, 2025 imeanza rasmi kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa wakazi wa mkoa wa Songwe na kwa kuanzia Wananchi wa wilaya ya Mbozi wameanza kununua mitungi hiyo kwa nusu bei.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amewapongeza REA pamoja na msambazaji, kampuni ya Oryx Gas kwa kuanza kugawa mitungi hiyo katika muda muhafaka na kutoa wito kwa REA na wasambazaji kuendelea kutoa elimu kuhusu usalama wa gesi; na faida ya matumizi ya nishati safi na salama kiafya na namna zinvyochangia katika utunzaji na uhifadhi mazingira.

“Mpango huu wa kusambaza mitungi ya gesi ni mzuri na kama mnavyofahamu; Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mama Samia Suluhu Hassan ni Mhamasishaji namba moja wa nishati safi siyo tu barani Afrika bali Duniani kote, kwa ujumla na sisi tunaoishi mikoa ya pembezoni, ndiyo waathirika wakubwa wa changamoto zinazotokana na matumizi ya nishati zisizo safi.” 

"Naipongeza REA kwa kuanza kutekeleza Mradi huu, nawapongeza pia Oryx Gas kwa kuwa sehemu ya ajenda ya kusambaza nishati safi kwa Watanzani. Huu ni uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa letu” amesema Mhe. Chongolo. 

Kwa upande wake, Meneja Mradi wa Nishati Safi mkoa wa Songwe kutoka REA; Bwana Vencha Maganga amesema, Serikali kupitia REA imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya kusambaza nishati safi ikiwemo gesi (LPG) katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji na kuwaomba Wananchi wa mkoa wa Songwe kuchangamkia fursa ya kununua mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku ambayo ni shilingi 20,000 tu kwa mtungi wa gesi wa kilo sita (6) na fedha inayobaki, inalipwa na Serikali.

"Lengo letu ni kutoa elimu na kuwawezesha Wamama ambao ndiyo watumiaji wakubwa wa nishati chafu ili wapate nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya nishati zisizo safi. Nawaomba Wananch wafike kwenye vituo vya kuuzia mitungi hiyo, wakiwa na Vitambulisho vya NIDA kwa ajili kununua mitungi hii pamoja na vifaa vyake kwa bei ya ruzuku ya shilingi (20,000/=) tofauti na ambavyo wangenunua kwa shilingi (40,000) na kuendelea hadi shilingi (60,000)”. Ameongeza Bwana Maganga.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi; Mhe. George Msyani amewapongeza Wananchi kufika kwenye kituo cha mauzo ili kununua mitungi hiyo ya gesi kwa bei ya ruzuku katika kitongoji cha Mlowo, wilayani Mbozi.

Wilaya zitakazonufaika na usambazaji wa mitungi hiyo ya gesi kwa mkoa wa Songwe ni pamoja Mbozi, Ileje, Momba na Songwe

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top