Sunday, August 9, 2020 Admin.Frank Mugogo 4470 News, Events, Announcements MWENYEKITI WA BODI YA NISHATI VIJIJINI ATOA WITO KUHUSU ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.Wakili Kalolo alitoa wito huo tarehe 07/08/2020 alipotembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.Alisema kuwa uharibifu unaofanyika katika miundombinu ya umeme ni pamoja na kuchoma moto nguzo, kuiba waya na vyuma vinavyoshikilia nguzo ili kuziwezesha ziwe imara. “Kuna watu wanaharibu miundombinu ya usambazaji wa umeme kwa kukata nyaya na vyuma vinavyofungwa katika nguzo na kutumia vifaa hivyo kufungia matela yanayokokotwa na ng’ombe” alisema.Aidha, alitahadharisha kuwa watakaokamatwa wakiharibu miundombinu ya usambazaji wa umeme watachukuliwa hatua za kisheria na alisema kwa kuwa miundombinu hiyo inajengwa vijijini, viongozi wa vijiji wanalo jukumu la kuilinda kwa kuwashirikisha wananchi.Imetolewa na:Mkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7Barabara ya MakoleS. L. P 2153Dodoma, TanzaniaBarua pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507 Tags Announcements News Events Share Print Switch article ENERGY ACCESS AND USE SITUATION SURVEY IN TANZANIA MAINLAND – APRIL 2020 Previous Article REA YAIBUKA NA USHINDI MAONESHO YA NANENANE MWAKA 2020 MKOANI SIMIYU Next Article