REA YAIBUKA NA USHINDI MAONESHO YA NANENANE MWAKA 2020 MKOANI SIMIYU
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka na ushindi wa pili katika kundi la Wakala wa Serikali katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Kutokana na ushindi huo, Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani alitoa pongezi kwa REA alipojumuika na Bodi ya Nishati Vijijini, Menejimenti na wafanyakazi wa Wakala pamoja na wadau wa nishati vijijini waliokuwa wakishangilia ushindi huo katika banda la Maonesho lililopo katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Akizungumzia ushindi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga aliwapongeza wafanyakazi kwa kushinda nafasi ya pili na kuwaagiza wabuni bidhaa na huduma nzuri zaidi za maonesho ambazo zitawezesha wananchi kupata taarifa kuhusu miradi ya kusambaza nishati vijijini na wadhamirie kufanya vizuri zaidi katika maonesho hayo ya kitaifa.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507