Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Rais Samia Apeleka Neema Tabora
Frank A. Mugogo 58

Rais Samia Apeleka Neema Tabora

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 19 wa kusambaza umeme katika vitongoji 180 utakaonufaisha Kaya 5,940 Mkoani Tabora.

Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle Novemba 07, 2024 Mkoani Tabora mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Paul Chacha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya Sinotec Company Ltd kutoka nchini China.

“Napenda kuwafahamisha wananchi wa Tabora kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta. Samia Suluhu Hassan ameridhia kiasi cha shilingi 19,057,015,682.55 kitumike kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 180 mkoani hapa na leo hii tupo hapa kumtambulisha mkandarasi anayetekeleza mradi huu,” alibainisha Mhandisi Dulle.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Chacha alimsisitiza Mkandarasi kuhakikisha anakamalisha kazi hiyo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa na aliipongeza REA kwa kuendelea kutimiza dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.

Akielezea utekelezaji wa mradi, Mhandisi Dulle amesema unatekelezwa ndani ya majimbo yote 12 ya mkoani humo na kwamba unatekelezwa kwa muda wa miaka miwili na utakamilika Mwezi Agosti, 2026 ambapo kila jimbo vitongoji 15 vitanufaika.

Amefafanua kuwa  hadi sasa vitongoji vilivyosambaziwa umeme ni vitongoji 1,323 kati ya vitongoji 3,749 na kwamba vitongoji vitakavyosalia vitasambaziwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha. 

Mhandisi Dulle amesema Mradi umelenga kusogeza miundombinu ya umeme kwa wananchi katika majimbo yote ili waweze kunufaika na nishati ya umeme katika kujiletea maendeleo hasa katika kuongeza thamani ya mazao, ufundi seremala, viwanda vidogo vidogo, mashine za kusaga na kukoboa sambamba na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.

“Vitongoji vitakavyonufaika ni kutoka katika Majimbo ya Sikonge, Urambo, Igalula, Tabora Kaskazini, kaliua, Ulyankulu, Bukene, Nzega Vijijini, Nzega Mjini, Igunga, Tabora Mjini na Manonga ambapo kila jimbo litapata vitongoji 15, Mashine umba 15 na wateja 495 na msongo mdogo (LV) umbali wa kilomita 30,” amefafanua Mhandisi Dulle.

Amesisitiza kuwa gharama ya kuunganishiwa umeme kwa wananchi ndani ya vitongoji hivyo ni shilingi 27,000 na kwamba mradi hautakuwa na fidia.

Mhandisi Dulle amesisitiza kuwa Wakala kwa kushirikiana na TANESCO unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchi nzima pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha wananchi kama ilivyo dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Naye Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya Sinotec Company Ltd, Mhandisi Alphred Kessy alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa watakamilisha mradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.


Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top