Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga
Frank A. Mugogo 205

Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 11.18 wa kusambaza umeme katika vitongoji 90 utakaonufaisha Kaya 2,970 Mkoani Shinyanga.

Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle amebainisha hayo Novemba 05, 2024 Mkoani Shinyanga mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anamringi Macha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya wazawa ya Derm Group (T) Limited ya Jijini Dar es Salaam.

“Tunamshukuru Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kiasi cha shilingi 11,184,759,397.2 kitumike kusambaza umeme katika vitongoji 90 Mkoani hapa, leo hii tumefika hapa kumtambulisha Mkandarasi na tayari maandalizi ya awali ya kutekeleza mradi yameanza,” alisema Mhandisi Dulle.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha aliipongeza REA kwa kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kwa utaratibu iliyojiwekea wa kutambulisha wakandarasi kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya kote nchini.

“Ujio wenu hapa ni habari njema sana kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya Mkoa wetu; pamoja na huduma zingine za jamii huduma ya umeme imepewa kipaumbele kikubwa na Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, umeme ni injini ya uchumi hili halina ubishi na sasa matumizi ya umeme yameongezeka, mahitaji kwa ajii ya majumbani na pia kiuchumi,” alisema Mhe. Macha

Alisema Mkoa wa Shinyanga unaendelea kukua kwa kasi na kwamba kwa sasa shughuli za kiuchumi zimeongezeka ikiwemo uwepo wa viwanda vidogo na vikubwa ambavyo vyote vinahitaji umeme.

“Hapa Shinyanga mbali na madini pia tunashughulika na kilimo cha mpunga na tungependa kuona mkulima akiongeza thamani ya mazao yake hukohuko unapozalishwa mpunga kwa kukoboa na kupata mchele na hapa faida itaongezeka sambamba na kuandaa ajira na fursa zingine vijijini,” alisema.

Aidha, alimtaka Mkandarasi kuhakikisha anatekeleza mradi kwa ubora na anakamilisha kwa wakati kwani tayari miundombinu ipo hivyo hakuna changamoto yoyote itakayokwamisha utekelezaji wa mradi.

“Tunafuraha kuona zipo kampuni za kitanzania zenye uwezo wa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo hii ya umeme ikiwemo kampuni hii ya Derm, tunatoa wito pia kutumia huduma na watoa huduma kwenye maeneo ya mradi, tutoe kipaumbele kwenye kazi zisizohitaji ujuzi mkubwa kwa wananchi wa maeneo ya mradi,” alisema.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kufikisha umeme katika vitongoji Mkoani humo, Mhandisi Dulle alisema Kati ya vitongoji 2,703 vilivyopo mkoani humo, vitongoji 930 vimefikishiwa umeme na kwamba vitongoji 90 vitakavyopata umeme awamu hii vitaongeza idadi ya vitongoji vitakavyokuwa na umeme Mkoani Shinyanga.

Alisema mradi unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 24 ambapo utekelezwaji wa mradi ulianza tarehe 3 Septemba, 2024 na utakamilika ifikapo tarehe 19 Agosti 2026 na kwamba vitongoji vitakavyobaki vitaendelea kusambaziwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mhandisi Dulle alibainisha kuwa mradi unatekelezwa katika majimbo sita kutoka katika Wilaya za Shinyanga, Kahama na Kishapu na kwamba kila jimbo vitongoji 15 vitanufaika.

“Mradi huu unalenga kupeleka umeme katika majimbo ya Shinyanga, Solwa, Kishapu,  Msalala, Ushetu na Kahama,” alisema Mhandisi Dulle.

Aidha, Mhadisi Dulle aliainisha hali ya upatikanaji wa umeme maeneo ya vijijini Mkoani humo sambamba na miradi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa ambapo alisema Kati ya vijiji 506 vilivyopo mkoani humo, vijiji 485 vimefikishiwa umeme ambayo ni sawa na asilimia 96 na kwamba vijiji 21 vilivyobaki vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili (REA3R2) chini ya Mkandarasi Tontan Project Technology LTD JV Group Six International.

Alisema vijiji hivyo vipo katika Wilaya ya Kahama na kwamba Mkandarasi anatarajiwa kukamilisha hivi karibuni.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«August 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
28293031123
45
Call for Proposal for Deployment of Stand-Alone Solar Home Systems (SA-SHS) in Remote Villages in Geita, Ludewa and Mbulu Districts

Call for Proposal for Deployment of Stand-Alone Solar Home Systems (SA-SHS) in Remote Villages in Geita, Ludewa and Mbulu Districts

The Rural Energy Agency (REA) is seeking proposals from qualified service providers for the supply, installation, and testing of Stand-Alone Solar Home Systems (SA-SHS) in eight remote villages across Geita, Ludewa and Mbulu districts. Those villages are located in remote areas with challenging geographical conditions, hence, impractical for grid extension.

Please find the attached documents:

•    Application Form for Supply and Installation of SA-SHS; and
•    Call for Proposals for Result Based Financing Installation of Stand Alone Solar Home Systems.

Read more
678910
111213
Kaya 3,255 kunufaika na majiko ya gesi ya ruzuku Wilaya ya Mlele

Kaya 3,255 kunufaika na majiko ya gesi ya ruzuku Wilaya ya Mlele

Wananchi Kijiji cha Usevya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kuhakikisha wanafikiwa na nishati safi ya kupikia kwa bei ya ruzuku.

Read more
1415
Viongozi wa Dini Mabalozi Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Viongozi wa Dini Mabalozi Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa wito kwa viongozi wa dini nchini kushiriki kikamilifu katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa lengo la kulinda afya na kuokoa mazingira.

Read more
1617
181920
Nishati Safi ya Kupikia Suluhu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Nishati Safi ya Kupikia Suluhu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Watanzania wameendelea kuhamasishwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Read more
21222324
25262728293031
1234567

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top