Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaendelea Kutekeleza kwa Vitendo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
Frank A. Mugogo 89

REA Yaendelea Kutekeleza kwa Vitendo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Serikali pamoja na Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia baada ya kutoa fedha zilizowezesha kufungwa kwa mfumo wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dr. Samia Suluhu Hassan mkoani Ruvuma.
 
Shule hiyo ya kisasa yenye wanafunzi zaidi ya 540 kwa sasa ipo katika Wilaya ya Namtumbo katika Mkoa wa Ruvuma ilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan jana Septemba 27.
 
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa shule hiyo, Mkurugenzi wa wa Mipango na Utafiti REA, Mhandisi Godfrey Chibulunje amemshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kutoa fedha zinazowezesha wakala kutekeleza miradi yake mbalimbali kwa wakati ikiwamo miradi ya nishati safi ya kupikia.
 
“REA tunaendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali pamoja na Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo na katika shule hii tumetoa Shilingi Milioni 38.2 kwa ajili ya kufungwa mifumo ya nishati safi ya kupikia tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanatumia kuni kupikia,” amesema Mhandisi Chibulunje.
 
Mhandisi Chibulunje amesema, REA itahakikisha shule mbalimbali zinafungwa mfumo wa nishati safi wa kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na kuongeza kuwa wakala huo umesaini mikataba ya zaidi ya Shilingi Bilioni 50 kuhakikisha taasisi zinazolisha watu zaidi ya 300 kama magereza na kambi za jeshi zinafungiwa mifumo ya nishati safi ya kupikia.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma kutoka REA, Bi. Martha Chassama amesema wakala umejipanga kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia huku akiendelea kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia.
 
“Mhe. Rais amekuwa ni kinara katika kuhakikisha anaokoa Watanzania waliokuwa wanafariki au kupata madhara ya kiafya kutokana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia. Na sisi kama REA tutaendelea kuhakikisha tunatoa elimu kwa umma ili lengo la kuhakikisha kufikia 2034 asilimia 80 au zaidi ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia,” amefafanua Chassama.
 
Awali akizungumza mara baada ya kuanza kutumia mfumo huo wa nishati safi ya kupikia, mpishi wa shule hiyo, Mzee Said Ruanda amesema kuwa awali wakati wanatumia kuni walikuwa wanatumia muda mwingi kuandaa chakula cha wanafunzi lakini pia jiko lilikuwa na moshi na joto sana.
 
“Kwa kweli kuna utofauti mkubwa sana toka tumeanza kupikia kwa kutumia gesi. Jikoni hamna moshi sana kama tulivyokuwa tunapikia kwa kuni lakini pia unaweza kupika ukiwa na nguo zako ulizokuja nazo na usichafuke tofauti na hapo zamani ilikuwa lazima ubadilishe nguo uvae nguo nyingine ili nguo zako ulizokuja nazo zisichafuke,” amefafanua mzee Ruanda.


Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top