Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri amepongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kupanda miti zaidi ya 2000 katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili ya Milembe.
Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji wa miti hiyo lililofanyika tarehe 4 Mei 2022 katika viwanja vya Hospitali ya Milembe ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Mazingira, Mhe. Shekimweri alisema kuwa ni wajibu wa wadau wote kuhakikisha miti hiyo inaota vizuri na kuwa itachangia kuweka mandhari nzuri inayoweza kuvutia utalii wa mazingira.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia wa REA, Mhandisi Advera Mwijage alihimiza utunzaji wa mazingira ili kuendelea kutunza vyanzo vya maji na kuweza kupata mvua za kutosha.
Naye Mkuu wa Idara ya Mazingira ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alisema kuwa Dodoma ya Kijani inawezekana kwa kuendelea kupanda miti na kuitunza ili iote na alitoa wito kwa wakazi wa Dodoma kupanda miti ya kivuli pamoja nay a matunda kwa ajili ya kutunza mazingira.
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507