Tuesday, May 24, 2022 Admin.Frank Mugogo 645 News, Events Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Atembelea Maonesho ya Wizara ya Nishati Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amewashauri Waheshimiwa Wabunge kutumia fursa ya Maonesho ya majukumu ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma kupata taarifa za utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini katika maeneo yao.Mhe. Ackson alitoa ushauri huo alipotembelea Maonesho hayo ya siku tatu yaliyoanza tarehe 23 Mei, 2022. “Tumepata fursa hapa ya kujua vijiji vingapi havijafikiwa umeme na vijiji vingapi vimefikiwa na huduma hiyo, wizara inajipanga kuelekea kwenye vitongoji. Kwa hiyo vitu kama hivyo ni vizuri, sasa Waheshimiwa Wabunge wamepata nafasi na wanaendelea kupata nafasi kwa sababu leo ni siku ya kwanza” alisema.Awali, Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba alisema lengo la Maonesho hayo ni kuwawesha Waheshimiwa Wabunge kupata majibu ya maswali waliyonayo kuhusu Wizara na Taasisi zake pamoja na huduma zinazotolewa.Naye Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi aliipongeza Wakala wa Nishati Vijijini kwa kazi nzuri katika miradi ya kusambaza umeme vijijini na kuwa amepata majibu ya changamoto za maeneo y Jimbo lake. “Nilikuwa na shida katika Kata za Mwampulu na Kasokola wamepeleka nguzo, nasubiri tuu mwezi ujao mambo yaende kwa kasi” alisema Mbunge huyo.Mkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7Barabara ya MakoleS. L. P 2153Dodoma, TanzaniaBarua pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507 Tags News Events Share Print Switch article REA WAADHIMISHA WIKI YA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI Previous Article Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali Kutekeleza Miradi ya REA Kusambaza Nishati Vijijini Next Article