Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Bilioni 15 Kusambaza Umeme Vitongojini Mkoa wa Pwani
Frank A. Mugogo 68

Bilioni 15 Kusambaza Umeme Vitongojini Mkoa wa Pwani

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Shilingi Bilioni 15 kutekeleza Mradi wa Kusambaza umeme kwenye vitongoji 135 Mkoani humo.

Ametoa shukran hizo leo Septemba 25, 2024 Ofisini kwake wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ya kumtambulisha Mkandarasi kampuni ya China Railway Construction Electrification Bureau Group Co. Ltd kutoka Nchini China atakayetekeleza mradi huo.

"Tunamshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Mkoa wa Pwani unakuwa Mkoa wa Kimkakati kwa kuwa na nyenzo zote muhimu za kuwaletea wananchi wake maendeleo ikiwemo hili la kusambaza umeme katika maeneo ya vitongoji," amebainisha Mhe. Kunenge.

Mhe. Kunenge ameipongeza REA kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo na amemsisitiza Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha mradi ndani ya muda kama ilivyo katika mkataba wake.

"Utaratibu huu wa kutambulisha Wakandarasi ni mzuri, unasaidia kutoa picha halisi ya tulipotoka, tulipo sasa na tunapoelekea, hongereni sana REA," alipongeza.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme maeneo ya vijijini Mkoani Pwani, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amesema Mkoa wa Pwani una jumla ya vijiji 417 ambapo vijiji 407 sawa na asilimia 98 vimeunganishwa na umeme.

Amesema vijiji 10 ambavyo havijafikishiwa umeme vipo kwenye maeneo ya delta katika Wilaya ya Kibiti (vijiji 5) na visiwa katika Wilaya ya Mkuranga (vijiji 3) na Mafia (vijiji 2).

"Vijiji hivi ambavyo bado havijapata umeme tayari mpango umeandaliwa vitafikishiwa umeme wa nishati mbadala kupitia miradi ya off-grid," alifafanua Mhandisi Olotu.

Kwa upande wa vitongoji, Mhandisi Olotu alisema Mkoa wa Pwani unajumla ya vitongoji 2,045 ambapo hadi sasa vitongoji 1,135 vimepata huduma ya umeme mbayo ni sawa na asilimia 55.6.

"Mkandarasi tunaemtambulisha leo atatekeleza mradi katika vitongoji 135 ikiwa na maana vitongoji 15 kwa kila jimbo katika majimbo yote tisa ya Mkoa wa Pwani kwa gharama ya shilingi 14,983,763,390, aidha vitongoji 775 vilivyobaki vitaendelea kupatiwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha,” alibainisha.

Alisema REA inatekeleza miradi kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika na kwamba utambuzi wa vitongoji hivyo vya mradi ulifanywa kwa kushirikisha Wabunge wa Majimbo yote Tisa Mkoani humo. 

Kwa upande wake Mkandarasi alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuwa atatakeleza mradi kwa mujibu wa mkataba na kwamba maandalizi yote muhimu amekwishafanya.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«November 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
28293031123
456
Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga

Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 11.18 wa kusambaza umeme katika vitongoji 90 utakaonufaisha Kaya 2,970 Mkoani Shinyanga.

Read more
78
REA Kufunga Mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia Shule ya Ruhinda

REA Kufunga Mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia Shule ya Ruhinda


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeahidi kujenga mifumo ya nishati safi ya kupikia pamoja na jiko katika shule ya Sekondari ya mchanganyiko ya Ruhinda iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.

Read more
910
111213

Report of the Controller and Auditor General on Financial and Compliance Audit for the Financial Year Ended 30 June 2023 for the Rural Energy Agency (REA)

Report of the Controller and Auditor General on Financial and Compliance Audit for the Financial Year Ended 30 June 2023 for the Rural Energy Agency (REA).

Read more
14
Call for Proposals to Supply Clean Cook Stoves for Promotions on Call Basis

Call for Proposals to Supply Clean Cook Stoves for Promotions on Call Basis

The Rural Energy Agency invites applications from qualified suppliers to submit proposals detailing the types of clean cooking solutions intending to supply clean cooking solutions across the country at subsidized rates. The proposal should also outline the actual costs and distribution expenses for providing these services in rural areas.

Read more
151617
18192021222324
2526272829301
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top