Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA yamtaka mwendelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Maguta mkoani Iringa kuongeza kasi
Frank A. Mugogo 450

REA yamtaka mwendelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Maguta mkoani Iringa kuongeza kasi

Serikali imemtaka Mwendelezaji wa Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji wa Maguta  uliopo katika Kijiji cha Masisiwe Wilayani Kilolo Mkoani Iringa kuukamilisha kwa wakati.

Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage ametoa maelekezo hayo Agosti 26, 2024 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao umefikia asilimia 95.

Mradi unatekelezwa na Mkandarasi ZECO ambaye Makao Makuu yake yapo Nchini Italia. Mwendelezaji ametakiwa kuhakikisha makubaliano ya utekelezaji wa mradi kati yake na  ZECO yanatekelezwa kwa wakati ili mradi ukamike ifikapo Desemba 2024. 

"Hatua iliyofikiwa inaridhisha; hakuna kikwazo kinachosababisha mradi uchelewe, Mkandarasi anapaswa kuhakikisha ifikapo Desemba mwaka huu awe amekamilisha na umeme umeingia kwenye Gridi ya Taifa," ameelekeza Mhandisi Advera. 

Mhandisi Advera amefafanua kuwa mradi umesanifiwa kuzalisha Megawati 2.4 na kwamba unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza inayoendelea hivi sasa itazalisha megawati 1.2. 
Amesema licha ya kuongeza umeme kwenye Gridi ya Taifa, mradi utazalisha ajira kwa wananchi wa eneo la mradi, utapunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa, ni rafiki kwa mazingira, utaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye maeneo mengi na hivyo kuleta chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Kilolo na maeneo mengine. 

"Kukamilika kwa mradi huu kutakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo haya na maeneo mengine pia; umeme ni injini ya uchumi hivyo tunatarajia kuona maendeleo makubwa baada ya kuanza uzalishaji wa umeme," amesema. 
Mhandisi Advera amebainisha kuwa mradi unatumia Nishati Safi na Salama kutokana na maporomoko ya maji hivyo ili uwe endelevu ametoa wito kwa kila mwananchi kulinda na kutunza mazingira ya maeneo ya vyanzo vya maji. 

"Umeme unaokwenda kuzalishwa hapa ni wa maporomoko ya maji, sasa tusipolinda mazingira yanayozunguka hivi vyanzo vya maji yaani hii Mito tutasababisha mradi ushindwe kutupa matokeo tunayoyatarajia," amesisitiza Mhandisi Advera. 

Akizungumzia utekelezaji wa mradi kwa ujumla, msimamizi wa mradi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lung'ali Natural Resources Co. Ltd inayosimamia mradi huo kwa niaba ya Kanisa Katoliki-Parokia ya Jimbo la Iringa, Padri Luciano Mpoma ameishukuru Serikali kwa mchango wake katika kuhakikisha mradi unakamilika. 

Amesema mradi unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Mitaji kwa ajili ya Maendeleo (UNCDF). 

"REA imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mradi unafanikiwa na unaleta manufaa yanayokusudiwa. Mara zote wamefika hapa kukagua na kutushauri tunawashukuru sana," amepongeza.

Miongoni mwa majukumu ya msingi ya REA ni pamoja na kuwezesha ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati Jadidifu ambayo ni Nishati Safi na Salama.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«February 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2627
Rais Samia Apeleka Neema ya Umeme Katika Vitongoji Lindi

Rais Samia Apeleka Neema ya Umeme Katika Vitongoji Lindi

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa shilingi bilioni 25.8 wa kusambaza umeme katika vitongoji 159 utakaonufaisha kaya 5,116 Mkoani Lindi.

Read more
2829
Shangwe Mtwara - Bilioni 15.3 Kusambaza Umeme Vitongoji 175

Shangwe Mtwara - Bilioni 15.3 Kusambaza Umeme Vitongoji 175

Wananchi wa vitongoji vya Msokole na Funguni Kijiji cha Mnazi Kata ya Nalingu Mkoani Mtwara wameishukuru Serikali kwa kuwapelekea mradi wa Umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao wamesema unakwenda kubadili maisha yao.

Read more
3031
Mkandarasi Northern Engineering Atakiwa Kuongeza Kasi Ya Ujenzi Wa Mradi Mtwara

Mkandarasi Northern Engineering Atakiwa Kuongeza Kasi Ya Ujenzi Wa Mradi Mtwara

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme katika Vitongoji 150 vya Majimbo 10 Mkoani Mtwara kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha Mradi kwa wakati.

Read more
1
2
Ukaguzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Mkoani Ruvuma

Ukaguzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Mkoani Ruvuma

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka Mkandarasi Kampuni ya CCC International Engineering Nigeria Ltd anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme katika Vitongoji 135 vya Majimbo 9 ya uchaguzi Mkoani Ruvuma kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha Mradi huo kwa wakati.

Read more
345678
9101112131415
16171819202122
2324252627281
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top