Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Wananchi waaswa kutunza mazingira
Frank A. Mugogo 2043

Wananchi waaswa kutunza mazingira

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewaasa wananchi kutunza mazingira na kulinda miundombinu pamoja na vyanzo vya maji ili kuendelea kupata huduma ya umeme pamoja na kuwa na miradi endelevu ya kufua umeme. 

Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage ametoa rai hiyo Wilayani Ludewa Agosti 27, 2024 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya matengenezo ya mitambo ya kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya mradi wa Lugarawa. 

Mradi wa Lugarawa unasimamiwa na Kampuni ya Madope na unamilikiwa kwa ushirikiano baina ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, Watumia Umeme Ludewa (wananchi) na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa. 

Mhandisi Advera alifafanua kuwa mradi unatumia Nishati Safi na Salama kutokana na maporomoko ya maji hivyo ili mradi uwe endelevu wananchi washirikiane kutunza mazingira. 

Akizungumzia dhumuni la ziara yake katika mradi, Mhandisi Advera alisema mradi huo wa Madope ni miongoni mwa miradi ya kufua umeme kwa kutumia Nishati Jadidifu inayowezeshwa na REA. 

"Nimefika hapa kukagua shughuli zinazoendelea za matengenezo ya mitambo, kama mnavyotambua REA inawezesha miradi hii; kuna fedha ya Serikali hapa; hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri na kuhakikisha uzalishaji unaendelea," alifafanua. 

Alisema zaidi ya wateja 5,000 walikuwa wanahudumiwa na mradi lakini tangu umesimama kutokana na hitilafu iliyojitokeza wateja hao kwa sasa wanahudumiwa na TANESCO kupitia miundombinu ya usambazaji iliyojengwa na REA. 

Alisema mara baada ya matengenezo kukamilika; umeme utakaozalishwa na mradi utaingizwa katika Gridi ya Taifa kupitia miundombinu iliyopo. 

Kwa upande wake Meneja wa Mradi, Mhandisi Masanja Kurwa alisema mradi uliwezeshwa na REA na kwamba ulianza rasmi kuzalisha umeme tarehe 30 Agosti, 2019 ambapo ulikuwa ukihudumia Vijiji 20 katika Kata 6 Wilayani humo. 

Alisema mradi ulisanifiwa kuzalisha Kilowat 1,700 lakini haukuweza kufikisha na hivyo Serikali ilielekeza kusimamisha uzalishaji ili kufanya maboresho ya mitambo ili kufikia lengo. 

"Tunaishukuru REA kwa kuendelea kutushika mkono tangu hatua za awali kabisa za ujenzi na hata sasa katika haya maboresho tunayofanya tayari tumepewa fedha na REA na sasa tunasubiri Mkandarasi akamilishe ili tuuze umeme kwa TANESCO," alisema Mhandisi Kurwa. 

Mhandisi Kurwa amesema wanamtarajia Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya ZECO mwenye makao makuu yake Nchini Italia kufika hapo kwa ajili ya maboresho na kwamba taratibu zingine zimekamilika.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«April 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
303112
REA Yatangaza Mafanikio Makubwa Ya Usambazaji Wa Nishati Vijijini

REA Yatangaza Mafanikio Makubwa Ya Usambazaji Wa Nishati Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetangaza mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini, huku ukieleza kuwa vijiji vyote nchini tayari vimefikishiwa umeme na sasa nguvu kubwa imeelekezwa katika vitongoji.

Read more
345
67891011
REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo

REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imewekeza jumla ya shilingi bilioni 12.1 katika miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Read more
12
1314151617
REA Yachochea Uwekezaji Mkoa Wa Mwanza – RC Mwanza

REA Yachochea Uwekezaji Mkoa Wa Mwanza – RC Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufikisha umeme katika vijiji pamoja na pembezoni mwa mji hali iliyochochea kuongezeka kwa uwekezaji maeneo ya vijijini.

Read more
1819
2021
Dkt. Mataragio Atembelea Banda la REA

Dkt. Mataragio Atembelea Banda la REA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio  akitazama hali ya usambazaji umeme vitongojini kupitia Mfumo maalum wa Mawasiliano uliyobuniwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwaajili ya kuonyesha hali ya usambazaji umeme na mipango iliyopo maarufu kama REA Digital Platform alipotembelea Banda la REA

Read more
22
Vitongoji Vyote Tanzania Bara Kuwa Na Umeme Ifikapo Mwaka 2030- Waziri Ndejembi

Vitongoji Vyote Tanzania Bara Kuwa Na Umeme Ifikapo Mwaka 2030- Waziri Ndejembi

Serikali imedhamiria kuhakikisha vitongoji vyote 64,359 vya Tanzania Bara vinafikishiwa umeme ifikapo mwaka 2030 ili kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii vitongojini pamoja na utoaji wa huduma bora katika maeneo hayo.

Read more
23242526
27282930123
45678910

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top