Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yatoa Mafunzo ya Nishati Safi kwa Makundi Maalum
Frank A. Mugogo 332

REA Yatoa Mafunzo ya Nishati Safi kwa Makundi Maalum

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imepongezwa kwa kuwezesha na kuhamasisha upatikanaji wa  nishati bora na salama kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji ili watanzania watumie nishati safi na salama nchini.

Pongezi hizo zimetolewa leo Oktoba 23, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuf wakati akifungua mafunzo ya elimu ya matumizi ya nishati safi kwa Makindi Maalum iliyofanyika mkoani Katavi.

Mhe. Yusuf amewapongeza pia TAMAVITA (Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania) kwa kushirikiana na REA katika uhamasishaji na kukubali kupewa mafunzo hayo kutoka REA ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ameongeza kuwa, Rais Samia ni kinara wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini na kuwapongeza TAMAVITA kwa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati zisizo safi na salama na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia.

Amesema matumizi ya nishati zisizo safi zinamadhara kwa afya ya binaadamu kupitia joto na moshi unaotokana na nishati hizo ambao unatoa kemikali ambayo sio salama kwa afya hivyo kila mmoja abadilike na amhamasishe mwingine katika hilo.

Naye, Mhandisi kutoka REA, Ramadhan Mganga amesema kuwa Wakala umeandaa mpango maalum wa kuwezesha taasisi zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya 100 kwa siku  kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Tunataka ifikapo mwaka 2034; 80% ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ya Kupikia, kwa manufaa yao na vizazi vijavyo," amesisitiza Mha. Mganga.

Kwa upande wake, Meneja wa Bishara kutoka Tango Energy Limited, Sunday Nyembele amesema kuwa jumla ya majiko banifu 60 yatauzws kwa TAMAVITA katika semina hiyo na majiko banifu 3,126 yatauzwa kwa wananchi wa mkoa wa Katavi.

TAMAVITA ni taasisi maalum kwa walemavu wasiosikia viziwi inayojushughulisha na shughuli za ujasiliamali pamoja na utoaji wa elimu mbalimbali katika jamii ya walemavu viziwi.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
1213141516
REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uko katika hatua za mwisho kukamilisha mradi mkubwa wa ufungaji wa taa 214 za barabarani katika Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Tanzania (SAUT); Jijini Mwanza, hatua itakayoboresha mazingira ya usalama na kujifunzia kwa wanafunzi 13,600. Mradi huo unaoangazia barabara na maeneo ya chuo kwa urefu wa kilomita 6.42, unalenga kujenga mazingira rafiki na yenye ubora wa hali ya juu ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao kwa urahisi wawapo chuo hapo, hususan nyakati za jioni na usiku.

Read more
1718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top