Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Waazimia Kuwaburuza Mahakamani Wahujumu Miundombinu ya Umeme Tandahimba
Frank A. Mugogo 349

Waazimia Kuwaburuza Mahakamani Wahujumu Miundombinu ya Umeme Tandahimba

Wenyeviti wa Serikali za vijiji na vitongoji Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara wamesema hawatakuwa na huruma kwa watakaobainika kuhusika na hujuma ya miundombinu ya umeme na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Wamesema hayo Oktoba 21,2025 wilayani humo kwa nyakati tofauti katika vitongoji vya Tripoli, Matogoro, Mpakani B, Mji Mwema na Mnianda wakati wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kuunganishiwa umeme inayoratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

“Tumepokea mradi wa umeme na ni kama lulu hatukutarajia, tutasimama imara kuhakikisha tunailinda miundombinu hii ya umeme ili isihujumiwe, isiharibiwe na wahalifu wachache wasiopenda maendeleo na amani ya vitongoji vyetu,”amesisitiza Mohamed Malota Mwenyekiti wa Kitongoji cha Matogoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti wa vitongoji wilayani Tandahimba.

Malota ameishukuru Serikali kwa kutimiza majukumu yake kwa wananchi na aliahidi kwa kushirikiana na wenyeviti wengine watahakikisha umeme unabadilisha maisha ya wananchi kwa kuwahamasisha kuutumia kujiletea maendeleo.

“Rai yangu kwa wananchi, mradi umefika muda mwafaka ni kipindi cha mavuno ya korosho sasa hivi, tuchangamkie fursa hii ya kuunganishiwa umeme kwa gharama ya 27,000 pekee ili tubadilishe maisha yetu,”ametoa wito Matola.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mji Mwema, Abdallah Hassan amewatahadharisha wananchi na kuwataka kuwa makini ili kuepuka kutapeliwa na vishoka wenye kuomba fedha kwa mwananchi ili wamfanyie mpango wa kuunganishiwa umeme na badala yake wafuate taratibu zilizoelekezwa na wataalam kutoka REA.

“Pasitokee mtu yoyote akawadanganya mumpe fedha, huo ni ukorofi na ni utapeli, hata Mwenyekiti mimi sihusiki na suala la mtu kuunganishiwa umeme sina mamlaka hayo kazi yangu mimi ni kushawishi Serikali kuleta mradi ukishafika kazi yangu imekwisha,” alitahadharisha Hassan

Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa vitongoji hivyo walipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuwaletea mradi huo ambao walisema unakwenda kubadilisha hali ya maisha yao.

"Sisi wanawake wa kitongoji cha mtogoro tunashukuru kwa huu mradi, tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuondolea giza, ametukomboa sisi akina mama wa hali ya chini, ametuondolea kero nyingi ikiwemo matumizi ya nishati isiyo safi,” alisema Sophia Ali mkazi wa Kitongoji cha Matogoro.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika kampeni hiyo walisema kuwa kufika kwa umeme katika kitongoji chao kutakwamua hali zao za maisha hasa ikizingatiwa kuwa wanajihusisha na shughuli mbalimbali za kujiongezea vipato.

“Tulikuwa tunapata shida hata kuchaji tu simu ilikuwa hadi twende mbali lakini kufika kwa umeme mambo yanakwenda kuwa mazuri mimi ni mbanguaji korosho maarufu hapa, tutatumia umeme kubangulia korosho tutaungana akina mama hapa na kuwa na mashine inayotumia umeme kubangua korosho,” alisema Shahara Mwandazi.

“Ninamshukuru Mama Samia kwa kuwatuma REA kutoka huko Dodoma hadi hapa Tandahimba mwisho wa Tanzania, tumeipokea REA kwa furaha, Mama Samia Mungu atakulipa kwa kuwatuma REA kufika hapa, hakika unatujali sana wananchi wako,” alisema Salima Mtawamba Mkazi wa Kitongoji cha Tripoli.

REA inafanya kampeni ya kuhamasisha wananchi kuunganishiwa umeme sambamba na kuhamasisha kuutumia kujiletea maendeleo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top