Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali inayo mikakati ya kuhakikisha inaongeza matumizi ya gesi ya kupikia nchini.
Ameyasema hayo leo wakati wa mkutano na wananchi wa Mbinga kuhusu nishati safi ya kupikia ambao uliambatana na ugawaji ma mitungi ya gesi Zaidi ya 1500 kwa wananchi wa eneo hilo.
“Mpaka sasa kupitia REA tumeshatoa mitungi ya ruzuku 83,500 yenye thamani ya bilioni 3.5 na mwaka huu wa fedha tutatoa mitungi mingine 452,445 yenye thamani ya bilioni 10 ikiwa nia yetu na dhamira yetu ni kupunguza matumizi ya gharama ya kwanza".
Aawali akitoa mada kuhusu hatua zilizokwishachukuliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutekeleza maono hayo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anayetaka kufikia 2030 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, Kaimu Meneja Msaidizi wa Kiufundi REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya amesema Wakala umesambaza zaidi ya majiko banifu 200,000 kwa wananchi.
Ameongeza pia Serikali kupitia REA imetenga Shilingi bilioni 9 kwa ajili ya kuwezesha taasisi zinazohudumia watu Zaidi ya 300 kutumia nishati safi ya kupikia.
Imetolewa na:
Iddy M. Mwema
imwema@rea.go.tz
Afisa Habari
REA