Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Taasisi Zote za Huduma za Kijamii Kuunganishwa na Umeme
Aodax K. Nshala 570

Taasisi Zote za Huduma za Kijamii Kuunganishwa na Umeme

REA Yapongezwa Kufikisha Umeme Katika Shule Vijijini

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa Taasisi zote zinazotoa huduma za kijamii kama shule na vituo vya afya pamoja na nyumba za ibada zitafikishiwa umeme.

Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo leo Julai 22 wakati akiwasha umeme katika Shule ya Sekondari Nyasa iliyoko katika Kijiji cha Chimate wilayani Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. 

“Sisi kama Wizara ya Nishati ni kuhakikisha tunaongeza tija katika taasisi hizi zinazotoa huduma kwa kufikisha umeme. Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anahangaika usiku na mchana kutafuta fedha za kuboresha maisha ya Watanzania kila siku na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha taasisi na maeneo yote yenye umuhumi yanafikiwa na umeme.

Tayari TANESCO na REA wamejidhatiti maeneo ambayo kuna taasisi za kijamii kama shule, vituo vya afya, makanisa, misikiti vyote vinafikiwa na umeme ili kuboresha huduma za kijamii katika Taifa letu,” amesema Naibu Waziri Kapinga.

Amesema kuwa uwepo wa umeme shuleni umesaidia hata kuongeza ufaulu kwa kuwa wanafunzi wamekuwa wakipata muda wa kujisomea hata usiku tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya miradi ya kusambaza umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) haijaanza.

Awali akitoa taarifa, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Eng. Robert Dulle amesema kuwa gharama za kufikisha umeme katika kijiji hicho ni shilingi Milioni 286.

Eng. Dulle ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma unajumla ya Vijiji 554 na mpaka kufikia Julai 2024, vijiji 542 sawa na asilimia 97.8 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi inayotekelezwa na REA huku akihamasisha wananchin kuchangamkia fursa za uwepo wa umeme vijijini kufanya shughuli za kiuchumi zitakazoboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nyasa, Mwalimu John Ndelwa ameipongeza REA kwa kuwafikishia umeme shuleni kwao na kuahidi kuwa watatumia fursa ya kuwepo umeme kuwafundisha wanafunzi masomo ya jioni na hivyo kuongeza ufaulu.

Ameongeza kuwa uwepo wa umeme utawawezesha kuwa na mitihani mingi ya majaribio kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kuchapa mitihani wenyewe shuleni tofauti na awali ambapo walikuwa wanalazimika kutumia gharama kubwa kwenda kuchapisha katika steshenari.

Imetolewa na:
Iddy M. Mwema
imwema@rea.go.tz
Afisa Habari
REA

Share

Print
«August 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
1011121314
REA Yaeleza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Kwenye Tamasha La Kizimkazi Mwaka 2026

REA Yaeleza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Kwenye Tamasha La Kizimkazi Mwaka 2026

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umefanikiwa kusambaza takribani mitungi laki saba ya gesi ya kupikia (LPG) nchini kote, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kasi wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Read more
1516
1718

Maombi ya Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unakaribisha waombaji wenye vigezo kuomba mkopo wa kuwezesha ujenzi wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu vya bidhaa za mafuta (petroli na dizeli) ili kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini.

Pamoja na tangazo hili, tumeweka viambatanisho vifuatavyo:
•    Tangazo la fursa ya mkopo wa ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta ya Petroli na Dizeli vijijini.
•    Mwongozo wa utoaji mkopo wa ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta vijijini.
•    Fomu ya Maombi ya Mkopo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la REA
Mtaa wa Medeli
P. O. Box 2153,
DODOMA, TANZANIA.

Read more
1920212223
24252627282930
31123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top