TAARIFA KWA WAKANDARASI WALIOSHINDA ZABUNI ZA KUTEKELEZA MRADI KABAMBE WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umekamilisha taratibu za zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Turnkey III). Mradi huu unahusisha kupeleka umeme wa gridi kwenye Vijiji 3559 katika Mikoa 25 ya Tanzania Bara. Hatua zinazofuata ni Wakandarasi walioshinda kupewa barua za tuzo (Award Letters) na kusaini mikataba kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa Mradi.
Utoaji wa barua hizi unafuatia kukamilika kwa mchakato wa kuwapata wazabuni watakaotekeleza mradi huo uliogawanywa katika mafungu (Lots) 29. Wazabuni wanaopewa barua wanatakiwa kukamilisha vigezo na masharti yaliyotajwa katika barua za tuzo kabla ya kusaini mikataba ya utekelezaji wa Mradi.
Aidha, Wakala umeandaa Mkutano maalum kwa Wakandarasi kwa ajili ya kuwakabidhi barua za tuzo (Award Letters). Mkutano huo utafanyika tarehe 18 Mei 2017 kuanzia saa 8 mchana katika Ukumbi wa Hazina uliopo katika Manispaa ya Dodoma.
Wazabuni wote walioshinda wanatakiwa kushiriki katika Mkutano huu.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Barabara ya Sam Nujoma, 14414
S. L. P 7990
Dar es Salaam.
Simu +255 22 2412001/2/3
Barua pepe: info@rea.go.tz