Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unashiriki katika Maadhimisho hayo ambayo yamebebwa na kaulimbiu isemayo "Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji".
Wananchi waliotembelea banda la REA pamoja na kupata elimu kuhusu matumizi sahihi ya nishati pamoja na miradi inayotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini, pia wamepata elimu kuhusu nishati safi ya kupikia.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma