Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Kuendelea Kuwezesha Waendelezaji wa Miradi ya Nishati Vijijini
Frank A. Mugogo 348

REA Kuendelea Kuwezesha Waendelezaji wa Miradi ya Nishati Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) utaendelea kutoa sapoti kwa waendelezaji wa miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme kote nchini ili kuwezesha wananchi wengi kufikiwa na huduma bora ya nishati ambayo inachangia kuinua uchumi wa wananchi pamoja na huduma za kijamii.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amebainisha hayo Mkoani Njombe Juni 17, 2025 kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony Mtaka alipofika ofisini kwake kuelezea ziara yake ya kukagua miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme mkoani humo.

"Njombe ni moja ya Mkoa ambayo imepokea sapoti kubwa kwenye uendelezaji wa miradi ya nishati jadidifu," alisema Mhe. Balozi Kingu.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Mtaka alimueleza Mhe. Balozi Kingu namna ambavyo anafarijika kwa sapoti inayotolewa na REA kwenye miradi hiyo na alisema kwa namna mkoa huo ulivyo bado zipo fursa nyingi za kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji ya mito.

"Jiografia ya mkoa huu inaruhusu kuwa na miradi mingi ya kuzalisha umeme na bahati nzuri wananchi wanao mwamko mkubwa katika kubuni na kuanzisha miradi ya kuzalisha umeme," alisema Mhe. Mtaka.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dorica Omary aliipongeza Bodi ya Nishati Vijijini (REB) kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na REA.

"Miongoni mwa miradi ambayo inatupa faraja hapa ni miradi ya REA, kwakweli mnafanya kazi nzuri, suala la umeme hapa tupo vizuri," alipongeza Judica.

Mhe. Balozi Kingu yupo Mkoani Njombe kwa ziara ya siku nne kwa lengo la kutembelea na kukagua uendelezwaji wa miradi mbalimbali inayowezeshwa na REA akiwa ameambatana na Wataalam kutoka Wakala wakiongozwa na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nishati Jadidifu na Mbadala, Mhandisi Advera Mwijage.

Mhandisi Mwijage alisema kuwa Mkoa wa Njombe kuna vyanzo saba vya kuzalisha umeme vyenye Jumla ya Megawati 6.8 ambavyo vimefadhiliwa na REA na vimeunganisha wateja zaidi ya elfu tano.

Akizungumzia miradi hiyo, Mhandisi Mwijage alisema mbali na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme, miradi hiyo pia ni rafiki wa mazingira kwa kuwa haizalishi hewa ya Ukaa.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«November 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
1234567

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top