Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaja na Mpango Kabambe wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini
Frank A. Mugogo 529

REA Yaja na Mpango Kabambe wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mpango wa kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu vya bidhaa za mafuta (petrol na dizeli) maeneo ya vijijini ili kuondoa madhara yatokanayo na njia zisizo salama.

Hayo yamebainishwa Julai 3, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam ndani ya Banda la Maonesho la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Afisa Upimaji wa REA, Hussein Shamdas.

"Katika kuhakikisha nishati bora na salama inapatikana maeneo ya vijijini REA imeendelea kutekeleza majukumu yake ikihakikisha inaandaa na kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo mradi huu wa kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vidogo vya bidhaa za mafuta maeneo ya vijijini," alisema Shamdas.

Alitaja baadhi ya kadhia inayowakumbuka wakazi wa maeneo ya vijijini kufuatia kutokuwepo kwa vituo vya bidhaa za petrol na dizeli katika maeneo yao kuwa ni pamoja na gharama kubwa za upatikanaji wa bidhaa hizo tofauti na bei elekezi ya Serikali.

Mbali na suala la gharama, Shamdas alisema wakati mwingine bidhaa hizo zimekuwa zikiadimika maeneo ya vijijini kutokana na umbali uliopo kutoka kwenye vituo vya mafuta pamoja na gharama kubwa za usafiri.

"Kwa sasa uuzaji na uhifadhi wa bidhaa hizi za mafuta ya petroli na dizeli kwa vijijini sio safi na salama maana wengi wanahifadhi mapipa na madumu ya plastiki ndani ya nyumba jambo ambalo ni hatari linaweza kusababisha mlipuko na kugharimu maisha ya wananchi lakini pia sio salama kwa vyombo vya moto vinavyotumia bidhaa hizo," alisema Shamdas.

Madhara mengine ambayo Shamdas aliyataja ni pamoja na athari za kiafya kutokana na kuvuta hewa isiyo safi na salama kutokana na kuhifadhi bidhaa hizo ndani ya nyumba pamoja, athari za kimazingira zinazotokana na kumwagika kwa kwa mafuta maeneo mbalimbali pamoja na kuikosesha Serikali mapato kwa kuwa wauzaji wengi wa bidhaa hizo vijijini hawalipi kodi na tozo mbalimbali za Serikali.

"Kwa kutambua athari hizi na kwa kuzingatia malengo ya Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015, ni wajibu wa Wakala kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa nishati na kwa bei nafuu katika maeneo yote ya nchi kwa njia iliyo salama," alibainisha.

Shamdas alitoa wito kwa wananchi kote Tanzania Bara kuchangamkia fursa ya kuomba mkopo huo ili kuweza kujenga na kuendesha vituo vya mafuta ambapo alisema mwananchi atapaswa kujaza fomu maalum na hatua zingine zitaendelea na kwamba mwongozo wa uombaji wa mkopo huo unapatikana kwenye tovuti ya wakaa ambayo ni www.rea.go.tz na pia kwa sasa mwananchi anaweza kutembelea banda la REA na kupatiwa mwongozo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
293012345
REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu

REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu

Timu ya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na timu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tarehe 03 Oktoba, 2025 wameanza zoezi la uhamasishaji kwa Wananchi ili wajiunge na huduma ya umeme kwenye vitongoji mbalimbali vya mkoa wa Simiyu.

Read more
6789101112
13141516171819
Zaidi ya Vitongoji 2,350 Mkoani Mtwara Vyafikishiwa Umeme

Zaidi ya Vitongoji 2,350 Mkoani Mtwara Vyafikishiwa Umeme

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umefikisha umeme katika vitongoji 2,354 kati ya vitongoji 3,421 Mkoani Mtwara huku ukiendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji vilivyosalia mkoani humo.

Read more
20
Newala Waipa Kongole REA Mradi wa Kusambaza Umeme Vitongojini

Newala Waipa Kongole REA Mradi wa Kusambaza Umeme Vitongojini

Wakazi wa vitongoji vya Chihanga, Mpilipili, Mkwedu na Majengo Wilayani Newala Mkoani Mtwara wameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufikisha umeme katika vitongoji hivyo.

Read more
2122
Tangazo Kwa Taasisi Zinazohudumia Watu Zaidi ya 100 Kuhusu Uhamasishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Tangazo Kwa Taasisi Zinazohudumia Watu Zaidi ya 100 Kuhusu Uhamasishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), chini ya Wizara ya Nishati, una jukumu la kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora na salama kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini upande wa Tanzania Bara.

Read more
23242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top