Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Watumishi REA Wapongezwa
Frank A. Mugogo 93

Watumishi REA Wapongezwa

Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wapongezwa kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii hali iliyopelekea mafanikio makubwa ya Wakala huo ikiwamo kufikisha umeme katika Vijiji vyote vya Tanzania Bara.

Pongezi hizo zimetolewa leo Novemba 14, 2025 na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Nishati, Bi. Ziana Mlawa wakati wa Kikao cha Pili cha Baraza la Wafanyakazi REA liliyofanyika katika ofisi za Wakala huo Jijini Dodoma.

"Sisi pale wizarani tunasema Wizara ya Nishati ni Umeme. Tunaona mnavyofanya kazi kwa bidii. Tupo tayari kushirikiana wakati wote, ili kuhakikisha mnafikia malengo yenu vizuri,"amesema Bi. Ziana

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Nishati vijijini (REA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Hassan Saidy, amesema mafanikio yaliyofikiwa na REA ni matokeo ya kufanya kazi kwa ushirikiano na bidi huku akiwataka watumishi kuendeleza umoja na kufanya kazi kwa bidii.

Akibainisha baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa ni pamoja na ongezeko la upatikanaji na uunganishaji umeme ambapo upatikanaji wa umeme umeongezeka kutoka asilimia 69.6 mpaka 78.1 kwa maeneo ya vijijini, huku kwa nchi nzima ukiongezeka kutoka asilimia 78.4 mpaka 85.5.

Mhandisi Saidy ameongeza kuwa, kwa upande wa uungaji wa umeme umeongezeka utoka asilimia24.5 mpaka 37.1 kwa maeneo ya vijijini.

Aidha, kwa upande wa matumizi ya nishati safi ya kupikia umeongezeka kutoka asilimia 8 mpaka 23.

"Sisi tuna amini REA imechangia ongezeko la matumizi ya nishati safi ya kupikia. Matumaini ya Watanzania hasa wale wanaoishi vijijini yapo kwetu sisi Wakala wa Nishati Vijijini. Tukafanye kazi kwa bidi kuwahudumia wananchi," amesisitiza Mhandisi Saidy.

Mwakilishi Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Taifa, Jonas Rwegoshora amesisitiza watumishi wa REA kuwa sehemu ya mabadiliko ya mafanikio ya taasisi hiyo na kuhimiza ushirikiano wa watumishi wote kuanzia ngazi ya chini mpaka juu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma
 

Share

Print
«December 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
242526
Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya  Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaanza kutekeleza mradi wa kutandaza nyaya za umeme (wiring) kwa wananchi kupitia miradi ya kusambaza umeme inayotekelezwa na wakala kote nchini.

Read more
27282930
123
Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Nishati Safi

Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Nishati Safi

Karibu katika Hafla ya Kusaini Mikataba ya Kufunga Miundombinu ya Nishati Safi katika Shule za Sekondari 52 pamoja na Chuo cha VETA.

Read more
4567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930311234

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top