Watumishi Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa Jijini Arusha Machi 8, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ambayo yalitanguliwa na Maonesho yaliyohamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Maadhimisho yalifanyikia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kuhudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka taasisi mbalimbali kote nchini.
Maadhimisho yalibebwa na Kaulimbiu ya "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji".
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma