Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaendelea Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo
Frank A. Mugogo 15

REA Yaendelea Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na jitihada mbalimbali za uelimishaji, uhamasishaji na usambazaji wa bidhaa za Nishati Safi za Kupikia katika Mikoa yote Tanzania Bara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la  kuhakikisha 80% ya Wananchi wanatumia Nishati Safi za Kupikia ifikapo Mwaka 2034.

Hayo yameelezwa Machi 7, 2025 Jijini Arusha na Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya wakati wa Maonesho ya Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani 2025.

"Tunashiriki kutoa elimu, kuonyesha bidhaa mbalimbali za nishati safi ya kupikia na kuhamasisha wananchi hususan akina mama kutumia nishati safi ya kupikia ili kurahisisha maisha yao sambamba na kulinda afya zao," alisema Mhandisi Yesaya

Alisema REA imeandaa program mbalimbali zinazolenga kumrahisishia maisha mwanamke hasa ikizingatiwa kuwa mwanamke ndiye kinara wa jiko.

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa kulinda afya za wananchi wake sambamba na kuhifadhi mazingira ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiriwa na matumizi ya Nishati chafu za kupikia zikiwemo kuni na mkaa na sasa mwelekeo ni kujikita katika matumizi ya Nishati Safi za Kupikia ambazo Serikali inafanya kila njia zifike kwa kila mwananchi kwa gharama anayoweza kumudu.

"Hii ni fursa adhim ambayo imetolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye kinara wa Nishati Safi ya Kupikia kwa wananchi wake, tunatoa rai kwa Watanzania kuchangamkia fursa hii," alisema Mhandisi Yesaya.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa REA, Bi Martha Chassama alitoa wito kwa wanawake kutembelea banda la Wizara ya Nishati ili kujifunza kwa undani umuhimu wa kutumia Nishati Safi ya Kupikia.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«March 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
242526272812
3456
Arusha Wavutiwa na Bidhaa za Nishati Safi ya Kupikia

Arusha Wavutiwa na Bidhaa za Nishati Safi ya Kupikia

Wananchi Jijini Arusha wamevutiwa na bidhaa mbalimbali za Nishati Safi ya Kupikia na wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kufikisha bidhaa hizo katika Maonesho yanayoendelea mkoani humo kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.

Read more
789
10
Watumishi Wanawake REA Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Arusha

Watumishi Wanawake REA Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Arusha

Watumishi Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa Jijini Arusha Machi 8, 2025.

Read more
111213141516
17181920212223
24252627282930
31123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top