Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Zaidi ya Bilioni 14 Kutekeleza Mradi wa Umeme Vitongojini Kagera
Frank A. Mugogo 94

Zaidi ya Bilioni 14 Kutekeleza Mradi wa Umeme Vitongojini Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Bilioni 14 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa  Umeme kwenye vitongoji 135 Mkoani humo katika majimbo yote.

Ametoa shukrani hizo Septemba 18, 2024 alipotembelea kitongoji cha Bushweka kijiji cha Mulahya Kata ya Katerero, kuzungumza na wananchi kwa niaba ya wakazi wa Mkoa wa Kagera akiwa pia ameambatana na ujumbe wa Wakala Wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na CCC International Nigeria Engineering Ltd Ambaye Ndie Mkandarasi wa mradi huo. 

Mhe. Fatma Mwassa amewasihi na kuwaasa wananchi wa Mkoa wa Kagera kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mkandarasi ili aweze kukamilisha utekelezaji wa mradi ndani ya wakati na kwa viwango vinavyokubalika.

Vilevile Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakala  kumsimamia Mkandarasi vema ili akamilishe mradi kwa wakati na  kwa viwango kama mkataba unavyomtaka ili kwa haraka huduma za umeme ziweze kuwafikia wananchi. 
 
Mhe. Fatma Mwassa amesema Mhe. Rais anaendelea kuboresha maisha ya wananchi wake kwa kasi ndio maana amemaliza kupeleka huduma za umeme kwenye vijiji vyote nchini na sasa anaelekeza nguvu kwenye vitongoji kwa kuhakikisha wanapata nishati safi.

Awali, Msimamizi wa miradi ya Wakala wa Nishati vijijini (REA) Kanda ya ziwa  Mhandisi Ernest Makale amesema mradi huo kwenye vitongoji unadhihirisha na kubainisha nia ya serikali ya kuhakikisha kila  kitongoji nchini kinakua na umeme ifikapo  2030.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«March 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
242526272812
3456
Arusha Wavutiwa na Bidhaa za Nishati Safi ya Kupikia

Arusha Wavutiwa na Bidhaa za Nishati Safi ya Kupikia

Wananchi Jijini Arusha wamevutiwa na bidhaa mbalimbali za Nishati Safi ya Kupikia na wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kufikisha bidhaa hizo katika Maonesho yanayoendelea mkoani humo kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.

Read more
789
10
Watumishi Wanawake REA Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Arusha

Watumishi Wanawake REA Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Arusha

Watumishi Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa Jijini Arusha Machi 8, 2025.

Read more
111213141516
171819
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Yahitimisha Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme Mkoani Njombe

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Yahitimisha Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme Mkoani Njombe

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekamilisha ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya Nishati Vijijini (REA) inayotekelezwa na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kwa upande wa REA ziara hiyo imehitimishwa katika kijiji cha Welela, Jimbo la Lupembe, ambapo kamati hiyo imepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wa vijijini kwa kasi inayostahili.

Read more
20212223
24252627
Mhandisi Saidy Awapongeza Watumishi wa REA

Mhandisi Saidy Awapongeza Watumishi wa REA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy amewapongeza Watumishi wa Wakala huo kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma hali iliyopelekea kukamilika kwa miradi inayotekelezwa na REA kwa wakati na katika ubora ulikusudiwa.

Read more
282930
31123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top