Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imeendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme vijijini na Septemba 20 imetembelea na kukagua miradi hiyo katika Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhe. Balozi Meja Jenereali (mstaafu), Jacob Kingu amesema ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za bodi hiyo kukagua usimamizi wa miradi ya nishati vijijini katika mikoa mbalimbali.
Mwenyekiti Kingu akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhe. Balozi Radhia Msuya wamemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi katika Wilaya ya Kahama kuhakikisha anaongeza kasi na kukamilisha mradi kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika ili kila kijiji katika Mkoa wa Shinyanga kifikiwe na huduma ya nishati ya umeme ili dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata maendeleo iweze kutimia.
Kwa niaba ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy ameahidi kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi kumaliza mradi huo kwa wakati kama maelezo ya bodi yalivyotaka na kumtaka mkandarasi TonTan kuongeza watu wa kufanya kazi na kuhakikisha anawalipa stahiki zao kwa wakati ili wawe na morali ya kufanya kazi kwa bidi kuhakikisha vijiji vyote vilivyobaki vinakamilika ndani ya mwezi huu wa Septemba.
Ruanda.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma