Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Benki ya Dunia Yaridhishwa na Utekelezwaji wa Miradi ya REA
Frank A. Mugogo 16

Benki ya Dunia Yaridhishwa na Utekelezwaji wa Miradi ya REA

Benki ya Dunia (WB) yaihakikishia ushirikiano Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika utekelezaji wa miradi ya Nishati kote nchini kwa ulinzi wa mazingira na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma Mei 16, 2025 na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Nishati Tanzania kutoka Benki ya Dunia, Dkt. Rhonda Antoine wakati wa kikao cha Ujumbe kutoka WB na REA kujadili hatua za utekelezwaji wa miradi ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, uendelezaji wa miradi ya nishati mbadala na mradi wa kusambaza umeme vitongojini kote nchini.

"Tunaipongeza REA; tunaahidi kuendeleza ushirikiano wetu kwa kazi kubwa inayofanya, tumeridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa wakati wote wa kutekeleza miradi, vigezo vimezingatiwa," alisema Dkt. Antoine

Akizungumza katika kikao hicho kilichokutanisha viongozi na wataalam kutoka REA na ujumbe huo wa Benki ya Dunia, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy alishukuru ushirikiano unaotolewa na benki hiyo katika kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali inayosimamiwa na REA.

"Tunashirikiana kwa karibu na Wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo WB katika kufanikisha utekelezaji wa miradi tunayoisimamia kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya Watanzania wote," alisema Mhandisi Saidy.

Alisema Serikali imeipa jukumu REA kutumia nyenzo na maarifa mbalimbali kuhakikisha umeme unafika kwenye vitongoji vyote nchini sambamba na kuhakikisha mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia unafanikiwa kwa kuhakikisha 80% ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Aliuhakikishia ujumbe huo kuwa REA itaendelea kusimamia vyema miradi iliyochini yake kama ambavyo miongozo mbalimbali ya WB inavyoelekeza.

Aidha, ujumbe huo wa WB uliipongeza REA kwa kuzingatia dhana ya usawa wa kijinsia wakati wote wa utekelezaji wa miradi pamoja na namna ambavyo inashirikiana na wadau kutoka Sekta Binafsi kutekeleza miradi.

Kikao hicho ni taratibu iliyowekwa na Benki ya Dunia kujadili hatua za utekelezaji wa miradi inayoifadhili na kufuatilia maendeleo ya utekelezwaji wake.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«May 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
567891011
12131415
Zaidi ya Bilioni 17 Kusambaza Umeme Vitongojini Singida

Zaidi ya Bilioni 17 Kusambaza Umeme Vitongojini Singida

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 17.39 wa kusambaza umeme katika vitongoji 120 utakaonufaisha Kaya 3,960 Mkoani Singida.

Read more
16
Mkurugenzi Mkuu REA Aisisitiza Bodi Mpya ya Zabuni Kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu

Mkurugenzi Mkuu REA Aisisitiza Bodi Mpya ya Zabuni Kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy ameielekeza Bodi mpya ya Zabuni (Tender Board) ya Wakala kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu ili kuleta tija katika kazi zake.

Read more
1718
19
Benki ya Dunia Yaridhishwa na Utekelezwaji wa Miradi ya REA

Benki ya Dunia Yaridhishwa na Utekelezwaji wa Miradi ya REA

Benki ya Dunia (WB) yaihakikishia ushirikiano Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika utekelezaji wa miradi ya Nishati kote nchini kwa ulinzi wa mazingira na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Read more
202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top