Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kijiji cha Nziga Kibaoni Wilayani Kilwa Chapata Umeme na Mitungi 231 ya Gesi Yagawiwa Kilwa Kaskazini
Frank A. Mugogo 84

Kijiji cha Nziga Kibaoni Wilayani Kilwa Chapata Umeme na Mitungi 231 ya Gesi Yagawiwa Kilwa Kaskazini

Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini Mhe. Francis Kumba  Ndulane amewasha umeme katika kijiji cha Nziga Kibaoni Tarafa ya Njinjo katika Jimbo la Kilwa Kaskazini na amepongeza  Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa namna ambavyo imeendelea kubadili vijiji kufanana na miji na pia  kuweza kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kuwepo kwa kupitia  nishati safi na salama.

Mhe. Ndulane ameyasema hayo tarehe 21 Septemba 2024 alipokuwa  akiwasha umeme na kugawa mitungi ya gesi katika kijiji cha Nzinga Kibaoni hili linakwenda sambamba na kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amewaasa wananchi nchini kuhama katika matumizi ya nishati isiyo salama ya kupikia na kuhamia katika matumizi ya nishatisafi ya kupikia.

Mitungi hiyo ya gesi imegawiwa kwa wananchi kijijini hapo na Serikali  kwa wajasiliamali, vijana na wanawake kupitia REA.

Akielezea madhara yapatikanayo kwa matumizi ya nishati isiyo salama ya kupikia ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa mifumo ya kiikolojia, magonjwa ya macho na mfumo  wa kupumua pamoja na ukatili wa kijinsia  na wananchi kukosa muda wa kushiriki shughuli za kijamii, kiuchumi  na kimasomo.

Amewataka wananchi wa kijiji cha nzinga kuchamkia fursa hii ya kuhama katika nishati isiyo salama na kujikita katika nishati safi ni rahisi kutumia ili kuokoa muda. 

Pamoja na mambo mengine amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani alidhamiria kuhakikisha kuwa huduma ya nishati hususani umeme inapatikana kila mahali nchini, amewaomba wananchi  kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais katika kuleta maendeleo nchini ikiwemo mawasiliano, maji na umeme pamoja na elimu.

Amewataka wananchi katika Kijiji cha Nzinga kuchamkia fursa ya umeme wa uhakika ambapo fursa nyingi za kiuchumi zitapatikana na umeme usitumike kuwasha taa tu bali utumike katika kuhakikisha unabadili maisha ya wananchi kwa kufungua mashine za kusaga na shughuli nyinginezo za kiuchumi

Akizungumzia mradi wa REA mzunguko wa  pili katika Jimbo la Kilwa Kaskazini mradi amesema mradi ulikuwa na vijiji kumi na sita (16), lakini mpaka leo hii  vijiji saba tayari vina umeme na vijiji vingine  tisa (9) vitaunganishwa kabla ya tarehe 30 Novemba mwaka huu. Nzinga ni kijiji kikubwa kuliko vyote katika Jimbo la Kilwa Kaskazini  kina idadi ya watu 9,500 kwa mujibu ya sensa ya mwaka juzi kupatikana kwa huduma ya umeme katika kijiji hiki kitasukuma maendeleo katika vijiji vingine na jimbo zima Kilwa Kaskazini. 

‘’Namshukuru Mkurugenzi Mkuu REA  kwa kuweza kutekeleza miradi yenye tija na inayoleta matunda   katika Jimbo letu la Kilwa Kaskazini na Wilaya nzima ya Kilwa na kuwataka REA kuhakikisha wanakamilisha miradi yote  ya REA mzunguko wa pili  ikiwemo miradi ya vitongoji  kumi na tano (15) ‘’ Amesema Mhe. Ndulane.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Injinia Hassan Saidy Kijiji cha Zinga ni moja ya kijiji kinachopata umeme kupitia REA lakini pia ndani ya Jimbo la Kilwa Kaskazini kwa mwaka huu  vitongoji  kumi na nne (15), vitapatiwa umeme amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuipatia fedha za kutosha REA ili kuweza kutekeleza miradi hii

‘’Nishati safi ya kupikia ni nyenzo muhimu kwani Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. DKT. Samia  Suluhu Hassan ni muasisisi Barani Afrika na Tanzania ambapo ametoa maagizo kuhakikisha kuwa wananchi  wa Tanzania wanahama kutoka katika matumizi ya nishati isiyo salama ya kupikia na kuhamia katika nishati safi ya kupikia, ambapo jiko la gesi na mtungi unaouzwa kwa kiasi cha shilingi 45,000 wananchi vijijini  watanunua kwa bei ya shilingi 20,000 huu ni mkakati mahsusi ambapo Serikali kupitia REA italipia kiasi kilichobaki’’ Injinia Saidy amesema.

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itagawa takribani mitungi 450,000 nchi nzima na  Wilaya ya Kilwa itapata takribani mitungi 3500 na itagawiwa sawa kwa majimbo ya Kilwa Kaskazini na Kilwa Kusini. 

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imegawa kiasi cha mitungi 231 katika vijiji vya Ndete Tarafa ya Kipatimo na kijiji cha Zinga Kibaoni Tarafa ya Njinjo Katika Jimbo la Kilwa Kaskazini ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mahsusi wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kuwa wananchi wanatoka katika matumizi ya nishati isiyo salama ya kupikia na kuhamia katika Nishati safi ya kupikia.


Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top