Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
BODI YA REA YAAGWA NA KUTUNUKIWA TUZO KWA UTUMISHI WENYE TIJA
Admin.Frank Mugogo 862

BODI YA REA YAAGWA NA KUTUNUKIWA TUZO KWA UTUMISHI WENYE TIJA

Na Veronica Simba - REA

Bodi ya Nishati Vijijini inayosimamia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imehitimisha muda wake kisheria na kupongezwa kwa kutekeleza majukumu yake kwa juhudi, weledi, uadilifu na uzalendo.

Akizungumza mwishoni mwa juma, katika hafla fupi ya kuwaaga wajumbe wa Bodi hiyo, Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali aliwaeleza kuwa Serikali inatambua mchango wao katika majukumu mbalimbali waliyotekeleza, hususani katika kuongeza hali ya upatikanaji umeme vijijini hadi kufikia asilimia 69.8.

Mahimbali ambaye alimwakilisha Waziri wa Nishati, alieleza majukumu mengine yaliyotekelezwa na Bodi hiyo kwa ufanisi mkubwa ni pamoja na kuongezeka uunganishaji umeme kwa wateja wa vijijini kutoka 584,639 hadi kufikia wateja 956,511 sawa na asilimia 63.6.

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni kusimamia kuongezeka kwa Mfuko wa Nishati Vijijini kutoka Shilingi Bilioni 1,337 hadi Bilioni 1,684 sawa na asilimia 26. Aidha, kuongezeka kwa michango ya wabia wa maendeleo kutoka Shilingi Bilioni 252 hadi Bilioni 560 sawa na asilimia 123 pamoja na kusimamia kikamilifu maslahi ya wafanyakazi wa Wakala.

Naibu Katibu Mkuu alieleza zaidi kuwa, Bodi ilisimamia kikamilifu utekelezaji wa jukumu la msingi la Wakala ambalo ni kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora vijijini ili kuboresha maisha ya wananchi waishio vijijini, kiuchumi na kijamii kupitia upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo kuifanya Serikali kutembea kifua mbele kwa mafanikio yaliyopatikana ambayo yameacha alama Tanzania na Afrika nzima.

“Kwa niaba ya Serikali, ninawashukuru kwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati Vijijini kwa uadilifu mkubwa na maslahi mapana ya Taifa. Kwa hakika, kazi hii ni ngumu na inahitaji watu wenye uadilifu na uzalendo wa hali ya juu kutekeleza majukumu haya kama mlivyofanya ninyi.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi, Wakili Julius Kalolo, alitoa shukrani kwa Serikali, Wabia wa Maendeleo, Wizara ya Nishati, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa REA, kwa ushirikiano wa hali na mali katika kuiwezesha Bodi kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Wakili Kalolo alifafanua kuwa, kitendo cha Serikali na Wabia wa Maendeleo kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya nishati vijijini kimeiwezesha Bodi hiyo kupata mafanikio yote iliyofikia.

Aidha, alisema kuwa ushirikiano uliotolewa na wafanyakazi wote wa REA, Wizara na Taasisi mbalimbali zinazohusiana na Wakala huo, umechangia kwa kiasi kikubwa kufikia mafanikio hayo.

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Wajumbe wenzake wa Bodi, Mkurugenzi Dailin Mghweno alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaamini na kuendelea kuwapa nafasi ya kuwatumikia Watanzania hadi walipohitimisha muda wao.

Naye Mkurugenzi Mhandisi Francis Songela aliahidi kuwa Wajumbe wote wa Bodi hiyo wataendelea kutoa ushirikiano kwa REA na Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha malengo yote yaliyopangwa kutekelezwa yanafikiwa.

“Tutaendelea kuwa Mabalozi wazuri na tuko tayari muda wote kutoa ushirikiano pale utakapohitajika,” alisisitiza Mhandisi Songela.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy aliielezea Bodi hiyo kuwa ya kipekee kutokana na kuwa yenye ushirikiano mkubwa kwa Wakala.

“Kwakuwa wanatoka sehemu mbalimbali, kila mmoja ametumia ujuzi na uzoefu wake kuhakikisha REA inasonga mbele zaidi na zaidi.

Katika hafla hiyo, Mgeni Rasmi aliwatunuku tuzo na vyeti maalum kama ishara ya kutambua utumishi wao uliotukuka ambao umeleta tija katika sekta ya nishati vijijini.

Wajumbe wa Bodi hiyo iliyoteuliwa Januari 31, 2019 na ambayo imehitimisha muda wake wa miaka mitatu kisheria ni Mhandisi Styden Rwebangila akiwakilisha Wizara ya Nishati, Dailin Mgweno (Umoja wa Walaji Tanzania), Mhandisi Francis Songela (Wabia wa Maendeleo), Louis Accaro (Sekta Binafsi), Frolian Haule (Vyama vya Ushirika) na CPA Oswald Urassa (Umoja wa Benki Tanzania).

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz

Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

Share

Print
«July 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
30
REA Yasambaza Mitungi na Majiko ya Gesi kwa Watumishi wa Gereza la Ukonga Dar es Salaam

REA Yasambaza Mitungi na Majiko ya Gesi kwa Watumishi wa Gereza la Ukonga Dar es Salaam

Serikali imesambaza kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza (Gereza la Ukonga) mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko yake 464 ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kama njia ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia nchini ambapo msisitizo ni angalau asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ifikapo Mwaka 2034.

Read more
1
Mhe. Rais Samia Apongezwa Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo

Mhe. Rais Samia Apongezwa Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo.

Read more
2
REA Yasambaza Mitungi, Majiko ya Gesi kwa Watumishi 461 wa Magereza Mkoa wa Mara

REA Yasambaza Mitungi, Majiko ya Gesi kwa Watumishi 461 wa Magereza Mkoa wa Mara

Katika kuendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imegawa jumla ya mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko ya sahani mbili 461 kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mara.

Read more
3
REA Yaja na Mpango Kabambe wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini

REA Yaja na Mpango Kabambe wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mpango wa kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu vya bidhaa za mafuta (petrol na dizeli) maeneo ya vijijini ili kuondoa madhara yatokanayo na njia zisizo salama.

Read more
4
Watanzania Watakiwa Kuachana na Dhana Potofu Kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni Gharama

Watanzania Watakiwa Kuachana na Dhana Potofu Kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni Gharama

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewasihi Watanzania kote nchini kuachana na dhana ya kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni gharama ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Read more
5
Vitongoji Vyote 64,359 Vitakuwa na Umeme Ifikapo 2030

Vitongoji Vyote 64,359 Vitakuwa na Umeme Ifikapo 2030

Imeelezwa kuwa hadi kufikia mwaka 2030 vitongoji vyote Tanzania Bara vitakuwa vimefikishiwa nishati ya umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
6
78
REA Yajizatiti Kufikisha Lengo la Taifa Kwenye Nishati Safi ya Kupikia

REA Yajizatiti Kufikisha Lengo la Taifa Kwenye Nishati Safi ya Kupikia

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema Wakala umejizatiti kuhakikisha 80% ya Watanzania wanatumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo mwaka 2034 kama ilivyoelekezwa katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Read more
910111213
14151617181920
21222324252627
28293031123
45678910

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top