Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Bukombe Waunga Mkono Jitihada za Rais Samia Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia
Frank A. Mugogo 551

Bukombe Waunga Mkono Jitihada za Rais Samia Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia

Wananchi kote Nchini wametakiwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutumia Nishati Safi ya Kupikia ili kuimarisha afya zao sambamba na kutunza mazingira.

Wito huo umetolewa Oktoba 10, 2024 Wilayani Bukombe na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage wakati wa Semina maalum ya Nishati  Safi ya Kupikia kwa wakazi wa Wilaya hiyo.

"Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa ajenda ya Nishati Safi ya kupikia na anafanya kila linalowezekana  kuhakikisha kila mwananchi anapata bidhaa za Nishati Safi za kupikia kwa gharama nafuu", alisema Mhandisi Mwijage.

Akizungumza wakati wa Semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mhe. Paskasi Muragili alimshukuru Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku kwenye bidhaa za nishati safi za kupikia suala ambalo alisema linakwenda kuimarisha afya za wananchi sanjari na kuhifadhi mazingira ambayo kwa kiasi kikubwa alisema yameathiriwa na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

"Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa Bukombe, tunakwenda kupokea mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku na hizi ni jitihada za Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza," alisema Mhe. Muragili. 

Aliwasihi wananchi wote watakaojipatia mitungi hiyo kuhakikisha inapomalizika wanajaza ili kuendelea kutumia nishati safi ya kupikia na si kurejea katika matumizi ya kuni na mkaa.

Akizungumza wakati wa Semina hiyo, Mhandisi Mwijage alisema Wakala umepewa jukumu la kuhakikisha bidhaa za nishati safi za kupikia zinafika katika kila pembe ya nchi ili kumuwezesha kila mwananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi na salama.

"Serikali kupitia REA imeanza na itaendelea kutoa ruzuku kwa bidhaa za nishati safi za kupikia lengo ikiwa ni kuhakikisha hakuna mwananchi anaachwa nyuma," alisema.

Mhandisi Advera alisema kwa bidhaa za mitungi ya gesi (LPG) Serikali imeingia makubaliano na watoa huduma ya kusambaza mitungi na katika mikoa yoye nchini ambapo kwa awamu hii kiasi cha mitungi 452,445 itatolewa kwa bei ya ruzuku katika kila Mkoa

"Kwa hapa Bukombe, mtoa huduma atakayesambaza mitungi ni Kampuni ya Manjis ambapo mitungi hii ya kilo sita ikiwa kamili na kichomeo na figa  itatolewa kwa shilingi 17,500 tu ambayo ni nusu bei, sawa na asilimia 50 tu ya gharama ili wananchi waweze kumudu gharama za nishati ya kupikia" Asilimia nyingine 50 inalipwa na serikali, alisema Mhandisi Mwijage.

Aliongeza kuwa upo mradi wa majiko banifu ambao wancho watachangia shingili elfu 5 hadi 15, na kwa sasa mradi huo upo katika hatua za uandaaji wa mikataba. Jumla ya majiko 200,000 yatasambazwa nchi nzima. Miradi mingine iliyotajwa ni pamoja na usambazaji wa gesi asilia,kuongeza uzalishaji wa mkaa  Mbadala,kuwezesha taasisi zinazolisha watu zaidi ya watu 100 kutumia nishati safi pamoja na kutoa elimu kwa umma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Mhe Yusuph Yusuph alipongeza uwepo wa semina hiyo ambayo alisema itaongeza uelewa miongoni mwa wanamchi kuhusiana na suala zima la nishati safi za kupikia.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top