Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Dkt. Mpango Atembelea Banda la REA
Frank A. Mugogo 74

Dkt. Mpango Atembelea Banda la REA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amepongeza jitihada za Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kuhakikisha wananchi wanafikishiwa Nishati Safi ya Kupikia.

Ametoa pongezi hizo Oktoba 23, 2024 Jijini Dar es Salaam alipotembelea Banda la REA katika Kongamano la 10 la Jotoardhi (ARGeo-C10).

Aidha ameielekeza REA kutazama namna ya kuweka ruzuku kwenye majiko yanayotumia nishati ya umeme kama inavyofanyika kwenye mitungi ya gesi na majiko banifu ili kuwawezesha wananchi wamudu gharama.

Alisema kwakuwa umeme umefika kila kona ya Nchi ni muhimu pia REA ikaandaa mpango maalum wa ruzuku katika majiko yanayotumia nishati ya umeme.

"Mmefanikisha kuweka ruzuku kwenye mitungi ya gesi na majiko banifu, mtazame namna ya kuwa na ruzuku kwenye majiko haya ya umeme ili kila mwananchi mwenye kuhitaji aweze kumudu gharama yake," alielekeza Mhe. Dkt. Mpango.

Awali akitoa maelelezo ya majukumu ya REA, Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya alimueleza Makamu wa Rais, Mhe. Mpango kuwa Wakala unatekeleza programu mbalimbali ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilima 80 ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ya Kupikia kama inavyoelekezwa katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).

Mhandisi Yesaya alisema Wakala umeingia makubaliano na wasambazaji wa mitungi ya gesi ambayo tayari inatolewa kwa bei ya ruzuku ya asilimia 50 katika mikoa yote Tanzania Bara ambapo kwa awamu ya kwanza mitungi ya 452,445 inatolewa.

Aidha alifafanua kuhusiana na ruzuku ya hadi asilimia 75 ambayo itatolewa katika majiko banifu ambapo alisema kwa kuanzia, takriban majiko 200,000 yatatolewa kwa bei hiyo ya ruzuku.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top