Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kilosa Wamshukuru Rais Samia Kuwafikishia Nishati Safi ya Kupikia
Frank A. Mugogo 920

Kilosa Wamshukuru Rais Samia Kuwafikishia Nishati Safi ya Kupikia

Wananchi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikishia mradi unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wa kusambaza majiko yaliyoboreshwa maarufu kama majiko banifu kwa bei ya ruzuku ya shilingi 14,700 kwa kila jiko.

Wametoa shukrani hizo Agosti 6, 2025 wakati wa uzinduzi wa mradi shilingi 9,400,799,626.7 wa kusambaza majiko banifu ambayo yatasambazwa kote nchini kwa bei ya ruzuku uliyofanyikia eneo la Stendi wilayani humo ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaka Hamdu akiwa mgeni rasmi.

“Rais Samia ni mkombozi wetu, sisi wajasiriamali ametusaidia sana, kwanza alituletea majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku na sasa tumepokea majiko haya banifu ambayo nayo yanakwenda kuwa msaada mkubwa kwa shughuli zetu za kila siku,” alisema Daines Samwel ambaye ni mjasiriamali la Stendi.

Naye Aisha Swai, mkazi wa Uhindini wilayani humo alisema majiko haya yanakwenda kupunguza gharama za maisha kwani hapo awali alikuwa akitumia zaidi ya shilingi 20,000 kununua mkaa kwaajili ya shughuli zake siku za mama lishe na kwamba kutokana na sifa ya majiko hayo ya kutumia mkaa mchache itamsaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli zake.

Akizindua mradi, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu alisema Wilaya ya Kilosa ni mnufaika mkubwa wa miradi inayosimamiwa na REA na aliipongeza kwa kuendelea kutekeleza na kusimamia maono na maelekezo ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo ya usambazaji wa umeme na usambazaji wa nishati safi ya kupikia.

“Kwa hapa Kilosa, tunashukuru sana, vijiji vyote vimefikishiwa umeme na kazi inaendelea ya kufikisha umeme kwenye vitongoji; leo hii tupo hapa kuzindua mradi mkubwa wa zaidi ya shilingi bilioni tisa wa majiko banifu yanayotolewa kwa bei ya ruzuku,” alisema Hamdu.

Alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia mradi huo ambao alisema ni suluhu ya uharibifu wa misitu inayoizunguka wilaya hiyo lakini pia ni mkombozi wa afya za wananchi hao ambao wamekuwa kwa kiwango kikubwa wakikata miti kwa ajili ya kuni za kupikia.

“Ndani ya wilaya ya Kilosa unaweza kusema kwa 100% wananchi wamekuwa wakitumia nishati isiyosalama, nishati ambayo siyo sahihi; tuliona njia nyepesi ni kutumia kuni lakini kumbe mambo yamebadilika misitu yetu inapaswa kubaki salama na afya zetu pia kutoathirika tena na moshi wa kuni,” alisisitiza Hamdu.

Akizungumzia mradi kwa ujumla wake, Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema kuwa REA imejipanga kikamilifu kuhakikisha lengo lililomo katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia linafikiwa.

“Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imetambua changamoto wanayopata wananchi wake na ndio sababu imeweka ruzuku kubwa ili kuwafikia wananchi wengi Zaidi. Miti inakatwa kwa wingi, akina mama na watoto wanapata madhara kiafya na ili kuondokana na madhara haya tumejuka na majiko banifu nchi nzima na kwa kuanzia kwa hapa Morogoro kila wilaya itafikishiwa majiko 1,195,” alifafanua Mha. Advera.

Alibainisha kuwa kampuni saba zimeshinda zabuni za kusambaza majiko banifu katika mikoa mbalimbali kote nchini na kwamba kila mwananchi mwenye kuhitaji jiko banifu kupitia mradi huo anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa ili kuiwezesha Serikali kutunza kumbukumbu na kupata takwimu halisi ya utekelezaji wa Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia.

Mhadisi Advera alibainisha kuwa mradi huo wa majiko banifu unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali na Jumla ya majiko 200,000 yatasambazwa nchi nzima.

Alisema REA itaendelea kutekeleza miradi ya Nishati Safi ya kupikia nchi nzima na kwa kutumia vyanzo na teknojia mbalimbali ili kuhakikisha watanzania wengi wananufaika.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
1213141516
REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uko katika hatua za mwisho kukamilisha mradi mkubwa wa ufungaji wa taa 214 za barabarani katika Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Tanzania (SAUT); Jijini Mwanza, hatua itakayoboresha mazingira ya usalama na kujifunzia kwa wanafunzi 13,600. Mradi huo unaoangazia barabara na maeneo ya chuo kwa urefu wa kilomita 6.42, unalenga kujenga mazingira rafiki na yenye ubora wa hali ya juu ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao kwa urahisi wawapo chuo hapo, hususan nyakati za jioni na usiku.

Read more
1718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top