Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Magereza Morogoro Yanufaika Na Mapinduzi Ya Nishati Safi Ya Kupikia
Iddy Mwema 241

Magereza Morogoro Yanufaika Na Mapinduzi Ya Nishati Safi Ya Kupikia

Mwenyekiti wa Bodi ya REA asema Asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia 2034 inawezekana

Jeshi la Magereza Mkoa wa Morogoro limeendelea kuhamasishwa matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwa ni sehemu ya Mkakati wa Serikali kuhakikisha Asilimia 80 ya wanatumia wahamie kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

 

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya nishati safi ya kupikia kwa Jeshi la Magereza mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (Mstaafu), Jacob Kingu amesema kuwa lengo la taifa la kufikia matumizi makubwa ya nishati safi ya kupikia linawezekana kutokana na uwepo wa vyanzo mbalimbali vya nishati hiyo.

 

Amesema wananchi wana nafasi ya kuchagua aina ya nishati safi kulingana na mazingira wanayoishi, ikiwemo gesi, mkaa mbadala pamoja na matumizi ya umeme kwa ajili ya kupikia.

 

“Inawezekana ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi za kupikia maana zipo nyingi" amesema Mwenyekiti Kingu.

 

Aidha, ameeleza kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kupeleka huduma ya umeme katika Vijiji na Vitongoji jambo litakalowezesha wananchi wengi zaidi kutumia umeme kama chanzo cha nishati safi ya kupikia.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP), Peter Anatory amesema mradi wa majiko ya nishati safi ya kupikia unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewezesha magereza 12 ya Mkoa wa Morogoro kunufaika na huduma hiyo.

 

Amesema kupitia mradi huo, magereza hayo yamepata majiko 15 yanayotumia mkaa rafiki kwa mazingira pamoja na tani 236 za mkaa huo, hali iliyosaidia kuongeza matumizi ya nishati safi katika taasisi za magereza.

 

“Mradi huu umekuwa kichocheo kikubwa kwa magereza katika kuhakikisha tunatumia nishati safi ya kupikia,” amesema Anatory.

 

Naye Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Samuel Aron Mwakatika amesema matumizi ya nishati safi yana mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wananchi, kulinda mazingira pamoja na kukuza uchumi wa taifa.

 

Amesema katika Chuo cha Udereva KPF Kingolwira, matumizi ya nishati safi yamesaidia kuokoa muda uliokuwa unapotea kwa wanafunzi kwenda kutafuta kuni.

 

“Katika chuo hiki tuna wanafunzi 381, hivyo zamani ilikuwa lazima kuwe na kundi la wanafunzi wanaokwenda kutafuta kuni jambo lililokuwa linapunguza muda wa kujifunza. Nishati safi imesaidia kuondoa changamoto hiyo,” amesema Mwakatika.

 

Aidha, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP), Nicostatus Magori amesema gereza hilo liliacha kutumia kuni kwa ajili ya kupikia chakula cha wafungwa tangu Desemba mwaka 2024 baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo wa kufungiwa mifumo ya nishati safi ya kupikia katika magereza.

 

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top