Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Wananchi Morogoro Wahimizwa Kufanya Wiring Kupokea Umeme
Iddy Mwema 231

Wananchi Morogoro Wahimizwa Kufanya Wiring Kupokea Umeme

Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro wamehimizwa kufanya maandalizi ya kupokea huduma ya umeme kwa kutandaza nyaya kwenye nyumba zao (wiring) ili kujitayarisha na miradi inayoendela ya umeme kwenye vitongoji.

 

Wito huo umetolewa leo Mei 19, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali (Mstaafu), Jacob Kingu wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya kufikisha umeme inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Mkoa wa Morogoro.

 

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti Kingu alitembelea Vijiji vya Ulundo pamoja na Mtego wa Simba ambako miradi ya REA ya kufikisha umeme kwenye vitongoji inaendelea kutekelezwa. Akiwa huko, aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanafanya wiring mapema ili miundombinu ya umeme kwenye vitongoji itakapokamilika waweze kuunganisha umeme.

 

“Umeme kwa sasa ni hitaji la msingi. Unabadilisha maisha ya watu, unaongeza uzalishaji na kuboresha huduma muhimu za kijamii kama afya na elimu,” amesema Balozi Kingu huku akitoa wito pia kwa taasisi za serikali kama shule na vituo vya afya kuhakikisha wanavuta umeme kwenye taasisi zao ili kuendelea kuboresha huduma kwa jamii.

 

Balozi Kingu alieleza kuwa serikali imeendelea kuwekeza katika kuboresha huduma za afya vijijini kwa kujenga vituo vya afya na zahanati pamoja na kupeleka vifaa tiba vya kisasa, lakini changamoto ya ukosefu wa umeme imekuwa ikikwamisha utoaji wa huduma bora.

 

Awalia, akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme Mkoa wa Morogoro, Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Kati, Mhandisi Aneth Malingumu amesema jumla ya Vitongoji 1,821 kati ya 3,391 tayari vimepatiwa umeme huku vitongoji 1,255 vikiwa kwenye hatua mbalimbali za kufikishiwa umeme.

 

Akiongea kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtego wa Simba Shomari Jaeka ameshukuru na kuipongeza serikali kwa kuweza kufikisha umeme katika kijiji chao na kuahidi kutumia msimu wa mavuno kuhamasisha wananchi katika kijiji chake kufanya wiring katika nyumba zao.

 

Kwa upande wake Mkandarasi anaetekeleza mradi wa HEP 2A kwa Mkoa wa Morogoro kupitia kampuni ya Sinotec, Kris Sun ameahidi watakamilisha mradi huo ndani ya muda wa mkataba.

 

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata huduma ya umeme kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top