Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mkandarasi Northern Engineering Atakiwa Kuongeza Kasi Ya Ujenzi Wa Mradi Mtwara
Mohamed Saif 288

Mkandarasi Northern Engineering Atakiwa Kuongeza Kasi Ya Ujenzi Wa Mradi Mtwara

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme katika Vitongoji 150 vya Majimbo 10 Mkoani Mtwara kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha Mradi kwa wakati.

Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme REA, Mha. Deogratius Nagu ametoa maelekezo hayo Januari 29, 2026 kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi katika Wilaya za Nanyumbu, Newala, Tandahimba na Masasi Mkoani Mtwara.

"Kasi ya utekelezaji wa mradi hairidhishi, jitahidini kuongeza kasi, tafuteni watoa huduma wa vifaa wengi ili ikitokea mmoja kachelewa mnachukua kwa mwingine," alielekeza Mha. Nagu.

Alisema kutegemea mtoa huduma mmoja mmoja kwa kila kifaa ni jambo la hatari kwani ikitokea amechelewa kugikisha vifaa site, kazi zinasimama na kuchelewesha kukamilika kwa mradi na aliwasisitiza kufanya kazi na Watoa huduma wanaotambuliwa na walio katika kanzidata za TANESCO ili kupata vifaa vyenye ubora unaokubalika.

Mha. Nagu alisema Mkandarasi wa Mradi Kusambaza Umeme atakayefanya vizuri anayo nafasi kubwa ya kupata kazi ya kutekeleza mradi mwingine.

"Mnapaswa kuwasimamia kwa karibu hawa wanaowasambazia vifaa mathalan huyu anayewauzia transfoma hakikisheni mnaweka mtu wenu maalum kiwandani kwa ajili ya kufuatilia kukamilika kwa taratibu za kusafirisha transfoma hizo kuja site," alielekeza Mha. Nagu.

Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Nothern Engineering, Mha. Christopher Masasi alikiri kuwepo kwa changamoto ya kucheleweshewa vifaa kutoka kwa watoa huduma na aliahidi kuongeza idadi ya watoa huduma watakosambaza vifaa kwa ajili ya mradi.

"Ni kweli hatuna changamoto zaidi ya hii ya kucheleweshewa vifaa na watoa huduma, tumepokea maelekezo na tunaahidi kuongeza kasi na leo hii tumepokea shehena ya vifaa hivyo kasi itaongezeka," alisema Mha. Masasi.

Aidha, kwa mujibu wa Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoani Mtwara, Mha. Daniel Mwandupe amesema Mkandarasi Nothern Engineering Works Limited anatekeleza mradi wenye thamani ya shilingi 16,717,407,821.65 utakaonufaisha Kaya 4,950.

Mha. Mwandupe amesema hadi sasa Mkandarasi amewasha vitongoji 40 na kuunga wateja 458 na anatarajiwa kukamilisha mradi ifikapo Agosti mwaka huu.

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top