Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Ukaguzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Mkoani Ruvuma
Mohamed Saif 342

Ukaguzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Mkoani Ruvuma

Mkandarasi atakiwa kuongeza Kasi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka Mkandarasi Kampuni ya CCC International Engineering Nigeria Ltd anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme katika Vitongoji 135 vya Majimbo 9 ya uchaguzi Mkoani Ruvuma kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha Mradi huo kwa wakati.

Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme REA, Mha. Deogratius Nagu ametoa maelekezo hayo Januari 31, 2026 kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi katika Vitongoji vya Mlimani Park na Liuli Chini Wilaya ya Songea Mkoani wa Ruvuma.

"Kasi ya utekelezaji wa mradi huu hairidhishi kwani hadi sasa Mkandarasi yupo asilimia 56 wakati alipaswa kuwa ametekeleza kwa asilimia 80 kwa maana kwamba amewasha vitongoji 43 kati ya vitongoji 135 ambavyo alitakiwa kuwasha,” amefafanua Mha. Nagu.

Mhandisi Nagu amemuelekeza Mkandarasi kumbadilisha Meneja wa Mradi, kuhakikisha anaongeza timu za mafundi na wataalam katika maeneo yote ya mradi na aongeze usambazaji wa vifaa vya mradi ikiwemo transafoma na nyaya ili afanikishe kukamilisha mradi mapema zaidi.

“Tumeongeza nguvu ya ufuatiliaji hapa na tumemueleza haturidhishwi na kazi yake; ahakikishe anazingatia maelekezo yaliyotolewa leo, tumejipanga kumsimamia kwa karibu zaidi na tunaamini hadi mwezi wa sita atakuwa amekamilisha mradi,” amesema Mhandisi Nagu.

Kwa upande wake Mhandisi wa Mradi, Erick Njau akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Mradi, Li Hongli amesema kuchelewa kwa mradi kunatokana na kuchelewa kufika kwa vifaa vya mradi hata hivyo aliahidi kutekeleza maelekezo na kukamilisha mradi kwa wakati.

"Ni kweli hatuna changamoto zaidi ya hii ya kucheleweshewa vifaa na watoa huduma, tumepokea maelekezo na tunaahidi kuongeza kasi,” amesema Mha. Njau.

Aidha, akizungumza kwa niaba ya Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Zakaria Ng’okorome amesema mradi unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 14.56 na kwamba utanufaisha wateja wa awali zaidi ya 5,400.

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top