Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mkurugenzi Mkuu REA Awataka Watumishi Kuwasimamia Wakandarasi Ili Vitongoji Vyote Vifikiwe Na Umeme Kwa Wakati
Mohamed Saif 181

Mkurugenzi Mkuu REA Awataka Watumishi Kuwasimamia Wakandarasi Ili Vitongoji Vyote Vifikiwe Na Umeme Kwa Wakati

Mkurugenzi Mkuu awaongoza Watumishi kuchagua Viongozi wapya wa Tawi la TUGHE na Klabu ya Michezo

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi, Hassan Saidy amewataka Watumishi wa Wakala kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kuhakikisha ndani ya muda uliopangwa wanafikisha umeme kwenye vitongoji vyote vya Tanzania Bara.

Ametoa maelekezo hayo Machi 30, 2026 Makao Makuu ya REA, Jijini Dodoma wakati wa kikao kazi na Watumishi wote, ambapo amesema baada ya kusaini Mradi mkubwa wa HEP II (B); Mradi wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 9,009 tarehe 17 Januari, 2026 na kuongeza kuwa kazi iliyombele ya kila Mtumishi ni kuhakikisha vitongoji hivyo vinafikishiwa umeme katika kipindi cha miaka mitatu yaani hadi 2029.

Mhandisi Saidy amesema kukamilika kwa Mradi huo wa HEP II (B) pamoja na miradi mingine inayoendelea kutafanya jumla ya vitongoji ambavyo tayari vitakuwa vimefikishiwa umeme kuwa takriban 51,000 kufanya vitongoji vitakavyobakia bila umeme na bila kuwa katika mradi wowote kuwa taklibani 13,000 ambavyo vimepangwa kuanza kusambaziwa umeme ifikapo mwaka 2030 kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2025 – 2030.

Awali ilielezwa kuwa Mradi huo wa HEP II (B) ni muendelezo wa jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) za kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa Wananchi wote wa Tanzania Bara.

Mradi huo unatarajiwa kutoa manufaa ya moja kwa moja kwa Wananchi kwa kuongeza upatikanaji wa huduma ya umeme vitongojini; kuboresha huduma za kijamii hususan katika sekta za afya, elimu na maji; kuwezesha matumizi ya umeme katika shughuli za uzalishaji na kuongeza kipato cha Wananchi pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa maeneo ya vitogojini pamoja na kuimarisha ustawi wa jamii.

 Aidha; Mhandisi, Saidy aliongoza Watumishi wa REA katika zoezi la kuchagua Viongozi wa TUGHE tawini hapo ambapo kwa kauli moja Watumishi waliwachagua Viongozi wao katika ngazi tofauti kama ifuatavyo: - Mwenyekiti wa Tawi ni Bwana Swalehe Kiloza, Katibu wa Tawi ni Mhandisi, Annet Malingumu; Mjumbe wa Halmashauri ya Tawi ni Bwana Issa Sabuni na Mwakilishi wa Kundi la Vijana, Mhandisi, Issac Sanga.

Viongozi wengine ni pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Wanawake ya Tawi la TUGHE REA ni kama ifuatavyo: - Mwenyekiti ni Bi. Wilhelmina Cheyo; Katibu ni Bi. Ruth Emmanuel; Mweka Hazina ni Bi. Aveline Wilfred; Wajumbe Kamati ya Wanawake ni Bi. Happiness Ndunguru na Mhandisi, Bertha Mwaituka.

Vilevile Watumishi wa REA pia walichagua Viongozi kwa upande wa Klabu ya Michezo ya REA ambapo itaongozwa na Bwana Selemani Mtunzy kama Mwenyekiti na Mwenyekiti Msaidizi ni Bwana Samwel Sumwa; Katibu ni Bwana Praygod Ng’hunda; Mweka Hazina ni Bwana Daniel Kisaka wakati Wajumbe wa Kamati Tendaji kwa upande wa Wanaume atakuwa Mhandisi, Thomas Mmbaga na kwa upande wa Wanawake atakuwa Bi. Beatrice Shelukindo.

Wakati huo huo Watumishi wa REA walishiriki kwenye zoezi la kuchagua Viongozi wa Chama cha Kijamii cha Wafanyakazi (REA Social Club) chenye lengo la kusaidiana wakati wa raha na changamoto mbalimbali. Viongozi wa Chama hicho waliochaguliwa ni kama ifuatavyo: Mwenyekiti ni Bwana Elias Gunzer; Katibu ni Bi. Theresia Mang’ung’ula; Mweka Hazina ni Bwana Shukuru Malebeto; Wajumbe wa Kamati Tendaji ni Bwana Pastory Mwijage na Bi. Emmy Chali.

Share

Print
«August 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
1011121314
REA Yaeleza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Kwenye Tamasha La Kizimkazi Mwaka 2026

REA Yaeleza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Kwenye Tamasha La Kizimkazi Mwaka 2026

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umefanikiwa kusambaza takribani mitungi laki saba ya gesi ya kupikia (LPG) nchini kote, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kasi wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Read more
1516
1718

Maombi ya Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unakaribisha waombaji wenye vigezo kuomba mkopo wa kuwezesha ujenzi wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu vya bidhaa za mafuta (petroli na dizeli) ili kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini.

Pamoja na tangazo hili, tumeweka viambatanisho vifuatavyo:
•    Tangazo la fursa ya mkopo wa ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta ya Petroli na Dizeli vijijini.
•    Mwongozo wa utoaji mkopo wa ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta vijijini.
•    Fomu ya Maombi ya Mkopo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la REA
Mtaa wa Medeli
P. O. Box 2153,
DODOMA, TANZANIA.

Read more
1920212223
24252627282930
31123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top