Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Imebeba Ajenda Ya Maendeleo Ya Watu Wa Vijijini– Mwenyekiti Kamati Ya Bunge Ya Nishati Na Madini
Mohamed Saif 159

REA Imebeba Ajenda Ya Maendeleo Ya Watu Wa Vijijini– Mwenyekiti Kamati Ya Bunge Ya Nishati Na Madini

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu, amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kusambaza umeme ili kuhakikisha wananchi wanaoishi pembezoni mwa miji na vijijini wanapata huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akizungumzia mafanikio ya Miradi ya kusambaza umeme katika mkoa wa Geita, Mhe. Mgalu alisema kuwa Miradi inayotekelezwa inalenga kupanua wigo wa huduma ya umeme katika vitongoji 15 kwa kila jimbo la uchaguzi HEP 2(A) pamoja na Mradi mkubwa wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 9,009 Tanzania nzima Geita ikiwemo.

Aidha; Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ameigaza Kampuni ya CCC Beijing Industrial & Commercial Co. Ltd ambayo inatekeleza Miradi mingi mkoani Geita kuhakikisha na hadi kufikia Machi 28, 2026 kukamilisha miradi ambapo kwa sasa utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 80 kukamilika haraka.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Wizara ya Nishati, Mhe. Salome Makamba amewapongeza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kuendelea kuisimamia vyema Sekta ya Nishati pamoja na ukaribu wao katika kufuatilia Miradi ya kusambaza nishati ya umeme hadi kwenye vitongoji.

“Kipekee naipongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kufika hadi kwenye vitongoji kuangalia utelekezaji wa Miradi ya kimaendeleo; ikiwemo hii ya kufikisha umeme kwenye kitongoji cha Elimu hapa katika kijiji cha Mshinde, hii ni mara ya kwanza kwa ugeni kama huu kufika mahali hapa”. Alisema Mhe. Salome Makamba

Katika taarifa yake ya awali; Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi, Jones Olotu ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa REA alisema mkoa wa Geita una jumla ya vijiji 486 na vitongoji 2,195, kupitia Miradi mbalimbali tayari huduma ya umeme imefika katika vijiji vyote 486 pamoja na vitongoji 1,193.

Mhandisi Olotu aliongeza kuwa ipo Miradi kadhaa ya kusambaza umeme kwenye vitongoji inayoendelea katika mkoa wa Geita ambapo baada ya kukamilika; mkoa wa Geita utakuwa na jumla ya vitongoji 1,895 ambavyo vitakuwa na huduma ya umeme na kubakia vitongoji 300 tu ambavyo vitapatiwa huduma hiyo, ifikapo mwaka 2030.

Mhandisi, Olotu amesema Serikali itaendelea kuhakikisha Wananchi wengi wa mkoa wa Geita wanafikiwa na huduma ya umeme ili kuchochea maendeleo na kuboresha maisha yao.

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top