Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Nishati Safi ya Kupikia Suluhu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi
Frank A. Mugogo 1084

Nishati Safi ya Kupikia Suluhu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Watanzania wameendelea kuhamasishwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
 
Wito huo umetolewa leo Agosti 18, 2025 Mkoani Rukwa na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Florian Haule wakati wa ugawaji wa mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko ya sahani mbili kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Rukwa unaotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
 
Akiwa ameambatana na Mjumbe wa Bodi hiyo, Stephen Mwakifwamba, Haule amewataka pia maafisa pamoja na askari wa jeshi hilo kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia kwa jamii inayowazunguka.
 
"Ni ukweli usiopingika kwamba Jeshi la Magereza hapo nyuma walikuwa ni wakala wakubwa wa uharibifu wa mazingira kwa kutumia kuni na mkaa kwa ajili ya kuandaa chakula cha wafungwa magerezani, hali iliyopelekea uharibifu wa mazingira hasa uoto wa asili. Lakini kwa sasa magereza yote yanatumia nishati safi ya kupikia.
 
Matumizi ya nishati safi ya kupikia yanakwenda kuokoa mazingira yetu na hivyo kupunguza madhara ya kiuchumi pamoja na kijamii ambayo yanatokana na mabadiliko ya tabia nchi. Niendelee kuwahamasisha mkawe mabalozi wazuri wa nishati safi ya kupikia ili tuendelee kulinda mazingira yetu," amesema Haule.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Vendeline Tesha amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha magereza yote katika Mkoa huo kufungwa mifumo ya nishati safi ya kupikia na kuwezesha pia askari wa jeshi hilo kupata majiko ya gesi na kuongeza kuwa kitendo hicho kitaenda kuongeza morali ya kazi kwa watumishi hao.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Emmanuel Yesaya amesema kuwa REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili maono ya Mhe. Rais pamoja na malengo ya Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao umebainisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia yanafikiwa.
 
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Afisa kutoka REA, Mhandisi Francis Manyama amesema kuwa kwa Mkoa wa Rukwa, jumla ya mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko ya sahani mbili 297 yamepangwa kugaiwa kwa watumishi wa jeshi la magereza katika Mkoa wa Rukwa.
 
Septemba 13, 2024, REA iliingia makubaliano ya utekelezwaji wa mradi wenye gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 35 na Jeshi la Magereza wa kuwezesha kutoa ruzuku kwa ajili ya kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa magereza yote ya Tanzania Bara.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
1213141516
REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uko katika hatua za mwisho kukamilisha mradi mkubwa wa ufungaji wa taa 214 za barabarani katika Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Tanzania (SAUT); Jijini Mwanza, hatua itakayoboresha mazingira ya usalama na kujifunzia kwa wanafunzi 13,600. Mradi huo unaoangazia barabara na maeneo ya chuo kwa urefu wa kilomita 6.42, unalenga kujenga mazingira rafiki na yenye ubora wa hali ya juu ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao kwa urahisi wawapo chuo hapo, hususan nyakati za jioni na usiku.

Read more
1718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top