Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yawezesha Vikosi Vya JKT Kukuza Matumizi Ya Nishati Safi
Iddy Mwema 60

REA Yawezesha Vikosi Vya JKT Kukuza Matumizi Ya Nishati Safi

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu ametoa wito kwa vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopata miradi ya nishati safi ya kupikia kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii zinazowazunguka.

Mwenyekiti Kingu ametoa wito huo leo Mei 5, 2026 wakati wa ziara ya Bodi hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia inaayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Kambi ya JKT ya Maramba mkoani Tanga.

Aidha, amesisitiza vijana wanaliopo kwenye kambi hizo za JKT kupatiwa mafunzo ya namna ya kutengeneza mkaa mbadala ili waweze kutumia ujuzi huo kujiajiri na kuwa mawakala wa kutengeneza mkaa mbadala pindi watakapomaliza mafunzo yao.

Kwa upande wake, akimwakilisha Mkuu wa JKT, Kanali Projest Rutaihwa aliishukuru menejimenti na Bodi ya REA kwa utekelezaji wa miradi nishati safi ya kupikia huku akiahidi kusimamia mradi huo unakuwa endelevu ili kuendelea kulinda mazingira pamoja na afya za wanaoandaa chakula.

Naye Luteni Kanali Thobias Ngailo, Meneja wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka JKT, ameeleza kuwa jumla ya vikosi 22 vimenufaika na fedha zilizotolewa na Serikali kupitia REA ambapo amesema mashine 30 kati ya 60 za kutengeneza mkaa mbadala zimeshasambazwa katika vikosi na zinaendelea kufanya kazi, hatua inayotarajiwa kuongeza uzalishaji na matumizi ya nishati safi kwa kiwango kikubwa.

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Balozi Meja Jenerali (Mstaafu), Jacob Kingu Mei 5, 2026 imetembelea na kukagua miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Maramba Mkoani Tanga.

Mhe. Mwenyekiti Kingu ametoa wito kwa vikosi vya JKT vilivyopata miradi ya nishati safi ya kupikia kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii zinazowazunguka ili kwa pamoja tuweze kufanikisha lengo lililowekwa na Serikali la ifikapo 2034, Asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Share

Print
«June 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
25262728293031
12
Bodi, Menejimenti REA Wabadilishana Uzoefu Na Ujumbe Kutoka Algeria

Bodi, Menejimenti REA Wabadilishana Uzoefu Na Ujumbe Kutoka Algeria

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamekutana na kufanya mazungumko na ujumbe kutoka nchini Algeria ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GISB Electric ambaye pia ni Makamu wa rais wa Kongani ya Viwanda vya Umeme Algeria (CIEL), Dk. Khelifa Mohammed.

Read more
34567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293012345

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top