Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Viongozi wa Dini Mabalozi Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
Frank A. Mugogo 28

Viongozi wa Dini Mabalozi Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa wito kwa viongozi wa dini nchini kushiriki kikamilifu katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa lengo la kulinda afya na kuokoa mazingira.

Rai hiyo imetolewa Agosti 13, 2025 katika Mji mdogo wa Majimoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe na Mtaalam wa Jinsia na Nishati wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt.Joseph Sambali wakati wa semina iliyoandaliwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya kwa viongozi wa dini kuwakumbusha nafasi zao katika jamii hususan  kuhusu umuhimu wa amani, utulivu na maadili katika jamii.

“Viongozi wa dini mnayo nafasi kubwa katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kutokana na nafasi yenu katika jamii; jambo hili mkilipa kipaumbele itasaidia kubadilisha fikra za jamii kuelekea kwenye matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia,” alisisitiza Dkt. Sambali.

Alifafanua kuwa REA inatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia ambao umeelekeza ifikapo mwaka 2034; 80% ya wananchi wawe wanatumia Nishati safi ya Kupikia.

Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Alhaj Majid Mwanga ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema viongozi wa dini ni kiungo muhimu katika kulinda amani, utulivu, maadili na uhifadhi wa mazingira kwa ustawi wa jamii nzima.

Akizungumza katika semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Shamim Mwariko alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa ya ununuzi wa majiko ya gesi (LPG) yanayouzwa kwa bei ya ruzuku ya shilingi 19,500 kwa ufadhili wa Serikali.

“Viongozi wa dini tunahitaji ushiriki wenu katika Kampeni hii ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa lengo la kulinda afya na kuokoa mazingira kwani kwa kufanya hivyo itachangia kuleta amani, utulivu na maadili katika jamii,” alisisitiza Mwariko
Kwa nyakati tofauti, wakichangia katika semina hiyo, viongozi wa dini waliahidi kuwa mabalozi wazuri wa Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni kuunga mkono ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

“Ajenda hii ya Nishati Safi ya Kupikia imekuja kwa wakati mwafaka kutokana na kuongezeka kwa mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa pia na ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa,” alisema Sheikh wa Wilaya ya Mlele, Awamu Muzamiru
“Tunaipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na viongozi wa dini, tumejadili mambo mengi na tunaahidi haya yote tuliyofahamishwa katika semina hii tutakuwa mabalozi wazuri kwa jamii”, alisema Mchungaji kutoka Kanisa la TAG Kijiji cha Kitupa, Paschal Katema.

Katika kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia (2024-2034), Wakala wa Nishati Vijijini unatumia njia mbalimbali katika kuelimisha, kuwezesha na kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika jamii.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«August 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
28293031123
45
Call for Proposal for Deployment of Stand-Alone Solar Home Systems (SA-SHS) in Remote Villages in Geita, Ludewa and Mbulu Districts

Call for Proposal for Deployment of Stand-Alone Solar Home Systems (SA-SHS) in Remote Villages in Geita, Ludewa and Mbulu Districts

The Rural Energy Agency (REA) is seeking proposals from qualified service providers for the supply, installation, and testing of Stand-Alone Solar Home Systems (SA-SHS) in eight remote villages across Geita, Ludewa and Mbulu districts. Those villages are located in remote areas with challenging geographical conditions, hence, impractical for grid extension.

Please find the attached documents:

•    Application Form for Supply and Installation of SA-SHS; and
•    Call for Proposals for Result Based Financing Installation of Stand Alone Solar Home Systems.

Read more
678910
111213
Kaya 3,255 kunufaika na majiko ya gesi ya ruzuku Wilaya ya Mlele

Kaya 3,255 kunufaika na majiko ya gesi ya ruzuku Wilaya ya Mlele

Wananchi Kijiji cha Usevya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kuhakikisha wanafikiwa na nishati safi ya kupikia kwa bei ya ruzuku.

Read more
1415
Viongozi wa Dini Mabalozi Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Viongozi wa Dini Mabalozi Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa wito kwa viongozi wa dini nchini kushiriki kikamilifu katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa lengo la kulinda afya na kuokoa mazingira.

Read more
1617
181920
Nishati Safi ya Kupikia Suluhu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Nishati Safi ya Kupikia Suluhu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Watanzania wameendelea kuhamasishwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Read more
21222324
25262728293031
1234567

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top