Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaandika Historia Mpya Korogwe
Mohamed Saif 181

REA Yaandika Historia Mpya Korogwe

Vitongoji vitano Mpale kufikishiwa umeme wa Gridi

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kamishna Mstaafu wa Uhifadhi, Mhe. William Mwakilema, amesema Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya nishati ya umeme ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika hafla ya kukabidhi mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa katika Kata ya Mpale Mei 6, 2026, DC Mwakilema ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kufanikisha ujenzi wa mradi huo mkubwa kwa sasa ambao  umekabidhiwa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa ajili ya usambazaji kwa wananchi.

Amesema kufikishwa kwa umeme huo katika vitongoji vya Ubiri, Kwemuhoyo, Milongwe, Kweulasi na Kwemhole ni hatua muhimu itakayosaidia kukuza shughuli za uzalishaji mali, biashara na huduma za kijamii, huku akiwataka wananchi kutumia fursa hiyo kujiletea maendeleo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Jacob Kingu, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuridhia utekelezaji wa mradi huo ambao umeleta suluhisho la kudumu la umeme katika eneo hilo.

Halikadhalika Mhe.Balozi Kingu amesisitiza umuhimu wa wananchi kuutumia umeme huo kuanzisha miradi ya maendeleo pamoja na kuchangamkia fursa za nishati safi ya kupikia ili kulinda mazingira.

Naye, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu, amesema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini na sehemu za pembezoni mwa miji wanapata umeme wa uhakika. 

Mha. Olotu ameongeza kuwa kabla ya kufikishwa kwa umeme wa Gridi ya Taifa, eneo hilo lilikuwa linatumia umeme wa jua kupitia kampuni ya Watu na Umeme tangu mwaka 2017 lakini Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 ilielekeza Serikali kubadilisha mfumo huo na kupeleka umeme wa gridi ya taifa ili kuwezesha matumizi makubwa zaidi ya umeme zitakazosaidia kuendesha mashine za viwandani na huduma nyingine muhimu.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Watu na Umeme Ltd, Dkt. Prosper Magali, amesema mradi wa awali wa umeme wa jua ulianza mwaka 2014 na uliweza kuhudumia kaya 254, lakini mahitaji ya sasa yameongezeka na hivyo kuhitaji umeme wa gridi.

Dkt. Magali ameishukuru REA kwa ushirikiano mkubwa hadi kufanikisha hatua ya sasa ya kukabidhi miundombinu hiyo TANESCO ambayo inakwenda kuboresha huduma  kwa wananchi.

Mradi huo unatajwa kuwa ni hatua kubwa ya maendeleo kwa wakazi wa Vitongoji vya Mpale, ambapo sasa wanatarajia kunufaika na umeme wa uhakika utakaowezesha ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha yao.

Share

Print
«November 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
26
REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

Wananchi wanaoishi katika Visiwa wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuwafikishia mifumo ya umeme jua kwa bei ya ruzuku hali iliyosaidia kuboresha maisha yao visiwani.

Pongezi hizo zimetolewa leo na wananchi wanaoishi katika Kisiwa cha Bezi kilichopo katika Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ilipotembelea kisiwani hapo kuona maendeleo ya mradi huo ambao unafadhiliwa na benki hiyo na kusimamiwa na REA katika visiwa 120 nchini.

Read more
2728
REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kufadhili miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha kaya na taasisi za umma zinanufaika na matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, hatua inayochangia kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na salama.

Read more
2930
Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Benki ya Dunia yapongeza miradi ya umeme vijijini kwa kuboresha maisha ya wananchi vijijini pamoja na huduma za kijamii.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mtaalam Mwandamizi wa Fedha kutoka Benki ya Dunia, Nkundwe Mwakiluma wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia iliyolenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
311
23
The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey provides data to inform energy-related programs and projects.

Read more
45678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top