Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Imefanya Kazi Kubwa ya Kufikisha Huduma za Nishati Vijijini
Mohamed Saif 256

REA Imefanya Kazi Kubwa ya Kufikisha Huduma za Nishati Vijijini

Waziri Ndejembi asisitiza ubunifu katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kufikisha umeme kwenye vijiji na maeneo ya pembezoni mwa miji iliyopelekea kukuza shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.

Pongezi hizo zimetolewa leo Novemba 28, 2025 wakati Mhe. Ndejembi alipokutana na kuzungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya REA kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na vitongojini pamoja na utekelezaji wa Mkakati wa nishati safi ya kupikia katika kikao kilichofanyika Ofisi za Makao Makuu ya REA jijini Dodoma.

"REA imefanya kazi kubwa na nzuri sana hapa nchini hususan katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Kipekee nachukua fursa hii kuipongeza sana Bodi ya REA, Menejimenti na Wafanyakazi kwa ujumla kwa kufanya kazi kubwa ya kupeleka umeme katika vijijini vyote nchini, " Amesema Mhe. Ndejembi.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, umeme vijijini haukuwa kama ilivyo leo na kuna watu walidhani kwamba kufikisha umeme kwenye vijiji vyote ni hadithi na haitowezekana lakini sasa vijiji vyote vimesambaziwa umeme hapa nchini na REA imefanya kazi kubwa.

Aidha, Mhe. Ndejembi ameipogeza REA kwa kushirikiana kwa karibu na wadau wengine wakiwemo TANESCO ambao kwa kiasi kikubwa wameshiriki katika kufikisha mafanikio ya Wakala katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Matarajio amesema kuwa, REA ni taasisi inayohakikisha kuwa Watanzania waliopo maeneo ya vijijini wanapata nishati safi na bora ya umeme ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija kupitia nishati hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu, Mhe. Balozi Jacob Kingu amesema kuwa REB itatoa ushirikiano wa kutosha kwa Waziri Ndejembi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za miradi ya umeme vijijini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy amesema kuwa vijiji vyote 12,318 tayari vimefikishiwa huduma ya umeme.

"Ufikishaji umeme kwenye vitongoji hadi sasa ni 39,003 kati ya 64,359 sawa na asilimia 61, vitongoji 2,562 vipo kwenye miradi inayoendelea (Densification 2A, HEP I, HEP IIA, HEP Lindi), " Amesema Mha. Saidy.

Halikadhalika mradi kusambaza umeme kwenye vitongoji (HEP 2B) wa vitongoji 9,000 utatekelezwa katika kila mkoa hapa nchini ambapo mradi utakuwa wa miaka mitatu na wateja wa awali wanatarajiwa kuwa 290,000.

Kuhusu nishati safi amesema REA inawezesha na kuhamasisha upatikanaji wa nishati safi kwa wananchi vijijini na pembezoni mwa miji, miradi hiyo inahusisha gesi asilia, LPG, majiko banifu na mifumo ya nishati safi katika taasisi.

Share

Print
«April 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
303112
REA Yatangaza Mafanikio Makubwa Ya Usambazaji Wa Nishati Vijijini

REA Yatangaza Mafanikio Makubwa Ya Usambazaji Wa Nishati Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetangaza mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini, huku ukieleza kuwa vijiji vyote nchini tayari vimefikishiwa umeme na sasa nguvu kubwa imeelekezwa katika vitongoji.

Read more
345
67891011
REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo

REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imewekeza jumla ya shilingi bilioni 12.1 katika miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Read more
12
1314151617
REA Yachochea Uwekezaji Mkoa Wa Mwanza – RC Mwanza

REA Yachochea Uwekezaji Mkoa Wa Mwanza – RC Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufikisha umeme katika vijiji pamoja na pembezoni mwa mji hali iliyochochea kuongezeka kwa uwekezaji maeneo ya vijijini.

Read more
1819
2021
Dkt. Mataragio Atembelea Banda la REA

Dkt. Mataragio Atembelea Banda la REA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio  akitazama hali ya usambazaji umeme vitongojini kupitia Mfumo maalum wa Mawasiliano uliyobuniwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwaajili ya kuonyesha hali ya usambazaji umeme na mipango iliyopo maarufu kama REA Digital Platform alipotembelea Banda la REA

Read more
22
Vitongoji Vyote Tanzania Bara Kuwa Na Umeme Ifikapo Mwaka 2030- Waziri Ndejembi

Vitongoji Vyote Tanzania Bara Kuwa Na Umeme Ifikapo Mwaka 2030- Waziri Ndejembi

Serikali imedhamiria kuhakikisha vitongoji vyote 64,359 vya Tanzania Bara vinafikishiwa umeme ifikapo mwaka 2030 ili kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii vitongojini pamoja na utoaji wa huduma bora katika maeneo hayo.

Read more
23242526
27282930123
45678910

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top