Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA na Shirika la Mzinga Kushirikiana Kuendeleza Teknolojia Za Nishati Safi ya Kupikia
Iddy Mwema 65

REA na Shirika la Mzinga Kushirikiana Kuendeleza Teknolojia Za Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Mzinga leo wamesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika Utafiti, Teknolojia, Uzalishaji na Usambazaji wa nishati safi ya kupikia.

 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga, Mhe. Balozi Luteni Jenerali (Mstaafu), Charles Lawrence Makakala, amesema utekelezaji wa mpango huo utakuwa msaada mkubwa kwa wanawake wa vijijini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kutafuta nishati kwa ajili ya kupikia.

 

“Akina mama wa vijijini wanapata adha kubwa kutafuta nishati ya kupikia. Madhara ya kiafya wanayoyapata wao pamoja na watoto wao ni makubwa kwa sababu watoto pia hushiriki katika shughuli za maandalizi ya chakula. Hatua hii itasaidia utekelezaji wa sera ya nishati safi lakini pia kuinua ustawi wa jamii na uchumi endelevu,” amesema Makakala.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (Mstaafu), Jacob Kingu, amesema ushirikiano huo utaongeza uzalishaji wa mkaa mbadala utokanao na mabaki ya mimea pamoja na uzalishaji wa majiko banifu kwa bei nafuu zaidi na hivyo kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

 

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema makubaliano hayo pia yanakwenda kuongeza aina za nishati safi za kutumika zenye gharama nafuu zaidi lengo likiwa kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

 

Mhandisi Saidy amesema kuwa kati ya Watanzania wanne, ni mmmoja tu ndo anatumia nishati safi ya kupikia. Hivyo kupitia ushirikiano huo unaokwenda kuongeza uzalishaji wa mkaa mbadala pamoja na majiko banifu, idadi ya Watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia itakwenda kuongezeka.

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mzinga, Brigedia Jenerali Mhandisi Seif Athuman Hamisi, amesema makubaliano hayo yatahusisha maeneo mbalimbali ikiwemo kufanya tafiti za kuboresha matumizi ya majiko na mkaa safi ili kuhakikisha teknolojia hizo zinakidhi mahitaji ya wananchi.

Share

Print
«June 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
25262728293031
12
Bodi, Menejimenti REA Wabadilishana Uzoefu Na Ujumbe Kutoka Algeria

Bodi, Menejimenti REA Wabadilishana Uzoefu Na Ujumbe Kutoka Algeria

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamekutana na kufanya mazungumko na ujumbe kutoka nchini Algeria ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GISB Electric ambaye pia ni Makamu wa rais wa Kongani ya Viwanda vya Umeme Algeria (CIEL), Dk. Khelifa Mohammed.

Read more
34567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293012345

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top