Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaendela Kusambaza Mitungi ya Gesi 16,275 Mkoani Simiyu
Frank A. Mugogo 19

REA Yaendela Kusambaza Mitungi ya Gesi 16,275 Mkoani Simiyu

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi, leo tarehe 18 Februari, 2025 amezindua rasmi zoezi la usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo 6 katika mkoa wa Simiyu na kutoa wito kwa Wananchi kuchangamkia fursa ya matumizi ya nishati safi kama njia mbadala ya kupunguza uharibifu wa mazingira, uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Mhe. Kenani amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kulinda afya za Watanzania pamoja na kutunza mazingira ambapo amewahamasisha Wananchi wa mkoa wa Simiyu kununua mitungi hiyo ya gesi pamoja na vifaa  vyake; mitungi inayosambazwa na kampuni ya ORYX Gas.

“Utekelezaji wa Mradi huu, unaunga mkono Mpango Mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo, lengo ni kuhakikisha kuwa angalau asilimia 80 ya Watanzania, wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.” Amesema Mhe. Kihongosi.

Usambazaji wa mitungi hiyo ya gesi unatekelezwa kwa pamoja kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na kampuni ya Oryx Gas Tanzania Limited, ambapo Wananchi wanapata fursa ya kukunua mitungi hiyo gesi ya kilo 6 kwa shilingi (20,000); bei ya ruzuku na kiasi kilichobaki kitalipwa na Serikali kupitia REA.

Naye Mhandisi wa Miradi ya Nishati Safi kutoka REA, Geofrey Gedo amesema Serikali, imedhamiria kuhakikisha Wanachi waliopo katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji wanatumia nishati safi ya kupikia.

“Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetenga fedha, takribani shilingi za Kitanzania milioni 325 kwa ajili ya utekelezaji miradi ya kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia (LPG) kwa mkoa wa Simiyu. 

“Mradi pia, unalenga katika kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kupunguza ukataji miti, ambapo takribani hekta laki 4 (400,000) hukatwa kila mwaka; wakati asilimia 63.5 ya kaya hutumia kuni kama chanzo kikuu cha nishati na asilimia 26.2 hutumia mkaa.

Mhandisi, Gedo ameongeza kuwa mitungi 16,275 itauzwa kwa bei ya punguzo ya asilimia 50 ambayo ni shilingi 20,000 katika mkoa wa Simiyu na kila wilaya ipata mitungi 3,255. 

Wilaya za mkoa Simiyu zitakazonufaika na usambazaji huo ni pamoja na wilaya ya Maswa, Bariadi, Itilima, Meatu na Busega.

Mhandisi, Gedo ameongeza kuwa ili Wananchi wapate mitungi hiyo wanatakiwa kuwa na Kitambulisho cha NIDA pamoja na shilingi (20,000) na watakapofika katika vituo vya kuuzia mitungi hiyo wataulizwa majina yao, jinsia; namba ya nida; mkoa, wilaya, kata, kijiji na kitongoji /mtaa anapoishi.

“Natoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha zoezi hili na baada ya kununua mitungi hii; wanunue na kuendelea kutumia nishati ya gesi.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma
 

Share

Print
«February 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
27
Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika

Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika - Misheni 300 ni kichocheo cha maendeleo ya nchi za Afrika na kichocheo cha utekelezaji wa Sera yake ya Taifa ya Nishati inayolenga kuendeleza nishati endelevu, uhifadhi na ufanisi.

Read more
2829303112
3456789
1011121314
REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe

REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na kampuni ya Oryx Gas Tanzania, tarehe 12 Februari, 2025 imeanza rasmi kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa wakazi wa mkoa wa Songwe na kwa kuanzia Wananchi wa wilaya ya Mbozi wameanza kununua mitungi hiyo kwa nusu bei.

Read more
1516
17181920212223
242526272812
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top