Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaendelea Kutekeleza kwa Vitendo Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia
Frank A. Mugogo 152

REA Yaendelea Kutekeleza kwa Vitendo Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia

Mkuu wa  Wilaya ya Ludewa Mhe. Olivanus Thomas akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo Oktoba 20,2025 amezindua rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa wilaya, Maafisa kutoka REA pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji vyake. 

Mhe. Olivanus amesema , lengo la uzinduzi  wa mradi huu ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi.

Mhe. Olivanus, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza Afya na kuhifadhi mazingira.

“Serikali imeweka ruzuku ya asilimia 85, kwa hiyo wakina Baba na kina Mama wa mkoa wa Njombe wajiandae kutumia majiko banifu,, kwetu sisi Mradi huu ni neema”. Alisema, Mhe. Olivanus.
                                                         
Akiwasilisha taarifa ya mradi  mbele ya Mkuu wa wilaya  na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo, Mhandisi wa miradi Kutoka wakala wa Nishati Vijijini, David Malima, amesema, mradi huu umekuja kwa lengo la kuimarisha na kuboresha Afya za wananchi, Mazingira, kukuza upatikanaji wa Nishati Safi na Endelevu, kupanua usambazaji wa nishati mbadala katika maeneo ya Vijijini na zaidi kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupikia , teknolojia za kisasa na bora za kupikia
Mradi huu unatarajia kugharimu kiasi cha zaidi ya TZS Milioni 285.3 kwa mkoa wa Njombe pekee na utafanikisha uuzaji na usambazaji wa majiko banifu 4,836.

Uuzaji na usambazaji wa majiko banifu utafanyika katika wilaya nne  (4) za mkoa wa Njombe ambazo ni wilaya ya Njombe, Ludewa, wanging’ombe na wilaya ya Makete ambapo kila wilaya majiko banifu 1,209 yatasambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.

Mikataba ya mradi huu ilisainiwa tarehe 25 Julai, 2025 kati ya REA na mtoa huduma kampuni ya Envotec Services Limited.

Mtoa huduma atasambaza na kuuza majiko banifu kwa bei ya ruzuku  katika wilaya zote nne. Gharama ya jiko moja ni TZS 59,000 lakini serikali imetoa ruzuku ya asilimia 85 sawa na TZS 50,150 hivyo mwananchi atanunua kwa gharama ya TZS 8,850 tu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«December 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
242526
Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya  Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaanza kutekeleza mradi wa kutandaza nyaya za umeme (wiring) kwa wananchi kupitia miradi ya kusambaza umeme inayotekelezwa na wakala kote nchini.

Read more
27282930
12
REA Imefanya Kazi Kubwa ya Kufikisha Huduma za Nishati Vijijini

REA Imefanya Kazi Kubwa ya Kufikisha Huduma za Nishati Vijijini

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kufikisha umeme kwenye vijiji na maeneo ya pembezoni mwa miji iliyopelekea kukuza shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo

Read more
34567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930311234

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top