Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA yapeleka Tabasamu Nsimbo
Mohamed Saif 220

REA yapeleka Tabasamu Nsimbo

Wananchi wachangamkia Majiko Banifu ya Ruzuku

Wananchi wa Kijiji cha Mtakuja Kata ya Kapalala katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameipongeza Serikali kwa kuweka ruzuku kwenye majiko banifu hatua ambayo wamesema inawezesha mwananchi wa kipato chochote kutumia Nishati Safi ya Kupikia.

Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti Desemba 19, 2025 wakati wa zoezi la usambazaji wa majiko banifu yanayouzwa kwa bei ya ruzuku kijijini hapo unaotekelezwa na Kampuni ya Tango Energy Limited chini ya uratibu na usimamizi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

“Tunaipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuweka ruzuku katika bidhaa za nishati safi ya kupikia ikiwemo haya majiko banifu; mpango huu utamfikia kila mwananchi hata yule wa kipato kidogo; Serikali imeamua kutusapoti nasi tumejitoa kama watanzania kuunga jitihada hizi za Serikali,” alisema Felix Milwano Mkazi wa Kijiji cha Kapalala

Kwa upande wake Nelia Fungameza alisema jiko banifu litampunguzia gharama za maisha kwani hapo awali alikuwa akitumia gunia moja la mkaa ndani ya mwezi mmoja lakini kutokana na ufanisi wa majiko hayo kama alivyoelezwa na wataalam ataweza kutumia gunia moja kwa zaidi ya miezi miwili.

Mbali na kupunguza gharama, Fungameza aliishukuru Serikali kwa dhamira yake ya kuboresha afya za wananchi wake kwani kwa kutumia majiko banifu alisema kwa namna alivyoshuhudia likifanya kazi halitoi moshi kama majiko mengine waliokuwa wakitumia hapo kabla.

“Haya majiko banifu mimi sifa zake nilielezwa na rafiki yangu yeye yupo Dar es Salaam, alinieleza ubora na ufanisi wake namna ambavyo yanafanya kazi na namna ambavyo yanaokoa gharama, leo nafarijika yamefika kwetu tena kwa bei ya ruzuku kwa hili naipongeza Serikali,” alisema Maiko Maseki.

Akizungumza wakati wa zoezi la uuzaji wa majiko hayo kwa bei ya ruzuku, Mtaalam wa Nishati na Jinsia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Joseph Sambali alipongeza mwitikio wa wananchi na aliwasisitiza kuwa mabalozi kwa wananchi wengine ambao hawakupata fursa ya kujipatia majiko hayo.

Alisema kuwa mwitikio huo mkubwa wa wananchi wa kujipatia majiko banifu kwa bei ya ruzuku kunadhihirisha kuwa uelewa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia katika kulinda afya na kuhifadhi mazingira umeongezeka miongoni mwa wananchi.

“Zoezi hili la uuzaji wa majiko Mkoani Katavi kwa bei ya ruzuku ya shilingi 7,500 linaendelea, nawasihi wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi waendelee kuchangamkia fursa hii kwani bei ya soko kwa jiko moja yaani bila ruzuku jiko hili huuzwa kwa shilingi 59,000,” alifafanua Dkt. Sambali.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Tango Energy Ltd, Musa Msofe alitoa wito kwa wananchi wanaofika kujipatia majiko banifu kwa bei ya ruzuku kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kuepuka usumbufu na kushindwa kupata huduma.

“Mwananchi anayefika hapa kujipatia jiko ahakikishe anakuja na kadi yake ya NIDA na huu ndio utaratibu nje ya hapo hatoweza kuhudumiwa; tumeanza rasmi uuzaji wa majiko hapa Nsimbo na tutakuwa na tutakuwa na vituo vitano vya uuzaji na tutatangaza ili kila mwananchi aelewe ratiba yetu,” alisema Msofe.

Alisema wamejipanga vyema kuhakikisha zoezi la uuzaji wa majiko hayo linakwenda kama ilivyoelekezwa na Serikali na kwamba kabla ya kuuza wanatoa elimu kuonyesha namna ambavyo majiko hayo yanafanya kazi sambamba na kumuonyesha mwananchi faida za kutumia majiko banifu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top