Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Prof. Msofe Avutiwa Na Miradi Ya REA, Apongeza Juhudi Za Kusogeza Nishati Kwa Wananchi
News

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo atembelea Banda la REA katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani

Prof. Msofe Avutiwa Na Miradi Ya REA, Apongeza Juhudi Za Kusogeza Nishati Kwa Wananchi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Peter Msofe, amepongeza jitihada za Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

 

REA Yawakaribisha Wananchi Kutembelea Banda Lake Siku Ya Chakula Duniani Tanga
News

REA kuonesha mchango wa nishati katika kukuza kilimo na uzalishaji wa chakula

REA Yawakaribisha Wananchi Kutembelea Banda Lake Siku Ya Chakula Duniani Tanga

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda lake katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Tanga Mjini, kuanzia Oktoba 10 hadi 16, 2026.

 

REA Yawanusuru Wanafunzi 700 Ruhinda Sekondari, Yawekeza Milioni 259 NIshati Safi Mkoa wa Kagera
National

Jumla ya shule 52 za Tanzania Bara zimeshanufaika na mpango huo wa REA

REA Yawanusuru Wanafunzi 700 Ruhinda Sekondari, Yawekeza Milioni 259 NIshati Safi Mkoa wa Kagera

 

Karagwe, KAGERA📍

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kupanua wigo wa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, baada ya kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya majiko ya kisasa na mifumo banifu mkoani Kagera, hatua inayolenga kulinda afya za wanafunzi na walimu pamoja na kutunza mazingira.

Uwekezaji huo umeshuhudiwa katika Shule ya Sekondari Ruhinda iliyopo wilayani Karagwe mkoani humo, ambapo takriban shilingi milioni 60 zimetumika kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la jiko la kisasa; usimikaji wa mifumo ya nishati safi ya kupikia pamoja na ununuzi wa tani 13 za kuni mbadala (Kuni poa).

Akizungumza baada ya kutembelea shule hiyo tarehe 12 Oktoba, 2026, Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Mbadala na Jadidifu kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage, alisema mradi huo umetekelezwa kupitia mkataba wa ruzuku uliosainiwa tarehe 20 Agosti, 2026 kati ya REA na Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ambao ndio walikuwa waratibu wa ujenzi huo.

Mhandisi, Advera alibainisha kuwa REA imeiwezesha shule hiyo ya Ruhinda ambayo inahudumia zaidi ya watu 100; kwa kujenga jiko ya kisasa na kusambaza tani 13 za kuni poa (kuni mbadala) kwa ajili ya kianzio, vyote vikiwa na thamani ya takriban shilingi milioni 60.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruhinda, Bwana Ambruse Abel, amemshukuru Wakala huo na Serikali kwa ujumla akieleza kuwa mradi huo umekuwa chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi takribani 700 wanaosoma shuleni hapo.

"Sasa hivi chakula cha wanafunzi kinapikwa katika mazingira bora, salama na kwa muda mfupi sana tofauti na zamani. Kipindi cha nyuma wakati wa mvua, chakula kilikuwa kinachelewa sana na afya za wapishi wetu zilikuwa hatarini kwa sababu ya moshi mkali," alisema Bwana Abel.

Aliongeza kuwa mradi huo umeisaidia shule hiyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwa zikitumika kununulia nishati za kiasili, ambapo awali takribani shilingi laki nane (800,000/-) zilitumika kila msimu kwa ajili ya kununulia kuni na mkaa.

Hadi sasa, jumla ya shule 52 za Tanzania Bara zimeshanufaika na mpango huo wa REA unaolenga kuhamisha taasisi za umma kutoka kwenye nishati zisizo safi na salama na kuelekea matumizi ya nishati salama na endelevu.

  • MWISHO –
RSS
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top