Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo
Mohamed Saif 31

REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo

Dkt. Homera aipongeza REA kwa utekelezaji wa miradi ya nishati Namtumbo

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imewekeza jumla ya shilingi bilioni 12.1 katika miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Hayo yamezungumzwa na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Juma Homera mara baada ya kuwasha umeme rasmi katika kitongoji cha Ujamaa na Kisutu vilivyopo wilaya ya Namtumbo mkoani humo  Aprili 10, 2026.

Dkt. Homera amesema, uwashaji wa umeme katika vitongoji hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme vijijini unawafikia wananchi wote ifikapo mwaka 2030

"Nampongeza sana Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy na timu yake kwa kuwezesha vijiji vyote 66 vya jimbo langu kupata huduma ya umeme na kama mnavyoona kasi bado inaendelea ya kupeleka umeme katika vitongoji 79 vilivyobakia vya jimbo hili," Amesema Dkt. Homera.

Halikadhalika Dkt. Homera ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa vitongoji hivyo kuchangamkia fursa kwa kufanya wiring ya umeme katika nyumba zao ili waweze kunufaika na huduma ya umeme ambayo imeletwa kwao kwa bei ya ruzuku ya shilingi 27,000 tu.

Kwa upande wake, Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme kutoka REA, Mha. Deogratius Nagu amesema kuwa Serikali imeweka jumla ya shilingi bilioni 12.1 katika miradi ya umeme wilayani Namtumbo kupitia miradi ya Ujazilizi na upanuzi wa miundombinu ya umeme ikiwemo miradi ya Densificationi 2C, HEP 2A na HEP 2B.

Ameongeza kuwa, Serikali  kupitia REA imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme kwa mafanikio makubwa ambapo vijiji vyote 66 vimefikiwa na huduma ya umeme wilayani Namtumbo.

"Kati ya vitongoji 424 vilivyopo, vitongoji 307 tayari vina umeme, na vitongoji 79 vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na vinapatiwa umeme pindi miradi hii itakapokamilika, hali itakayofikisha upatikanaji wa umeme hadi takribani asilimia 91 ya vitongoji vyote, Aidha, vitongoji 38 vilivyobaki vipo katika mipango ya kupelekewa umeme, ambapo mpaka 2030 vitongoji vyote vitakuwa na umeme" Amesema Mha. Nagu.

Naye, Msimamizi wa Miradi Mkoa wa Ruvuma Mha. Hamis Mrope amesema kuwa umeme huo utachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuongeza fursa za biashara, kuimarisha huduma za afya na elimu pamoja na kuboresha maisha ya wananchi.

Share

Print
«April 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
303112
REA Yatangaza Mafanikio Makubwa Ya Usambazaji Wa Nishati Vijijini

REA Yatangaza Mafanikio Makubwa Ya Usambazaji Wa Nishati Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetangaza mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini, huku ukieleza kuwa vijiji vyote nchini tayari vimefikishiwa umeme na sasa nguvu kubwa imeelekezwa katika vitongoji.

Read more
345
67891011
REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo

REA Yawasha Umeme Vitongoji 307 Namtumbo

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imewekeza jumla ya shilingi bilioni 12.1 katika miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Read more
12
13141516171819
20212223242526
27282930123
45678910

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top