Monday, July 17, 2017 Admin.Frank Mugogo 12769 News UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA MWANZA Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Mwanza. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 13/07/2017 katika kijiji cha Nyamatala, Kata ya Ngula, Wilaya ya Kwimba alikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuunganishiwa umeme. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi.Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Mwanza utahusisha vipengele vyote vitatu. Mradi huu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 174 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 30.37. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Aprili 2019. M/s NIPO Group Limited ni mkandarasi atakayetekeleza Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa Mwanza.Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika Mwaka 2019 ambapo vijiji 169 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya Mkoa wa Mwanza ifikapo Mwaka 2021.Imetolewa na:Mkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2Barabara ya Sam NujomaS. L. P 7990Dar es Salaam, TanzaniaBarua Pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003Nukushi: +255 22 2412007 Tags News Share Print Switch article UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA GEITA Previous Article UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA SIMIYU Next Article