Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa
Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Tanga. Mgeni rasmi Katika
uzinduzi huo uliofanyika tarehe 06/03/2017 katika kijiji cha Zingibari Wilaya ya
Mkinga alikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.
Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension,
Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji
ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji
havikuunganishiwa umeme. Kipengere-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa
nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi ambayo ni vigumu kufikiwa
na umeme wa gridi yakiwemo maeneo ya Visiwa.
Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa
Tanga utahusisha vipengele vyote vitatui. Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini
Awamu ya Tatu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali
itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 166 kwa gharama ya Shilingi Bilioni
26.1. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza imeanza Mwezi Februari 2017 na
inatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2019.
Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika mwaka 2019 ambapo
vijiji 244 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya
mkoa wa Tanga ifikapo Mwaka 2021.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania
Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007